Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man United, uwanja mpya mipango yaanza kukwama

Muktasari:

  • Ramani ya mwanzo ilikuwa inaonyesha uwanja mpya wa Man United utakuwa na paa kubwa la mfano wa “mwavuli,” na ilizua mjadala mkubwa na wengi walisifia lakini sasa mpango huo unaelekea kufeli.

MANCHESTER, ENGLAND: MANCHESTER United inadaiwa kuachana na mpango wa awali wa kujenga uwanja wenye paa la kisasa na la aina yake baada ya kukumbana na matatizo makubwa katika ununuzi wa ardhi.

Ramani ya mwanzo ilikuwa inaonyesha uwanja mpya wa Man United utakuwa na paa kubwa la mfano wa “mwavuli,” na ilizua mjadala mkubwa na wengi walisifia lakini sasa mpango huo unaelekea kufeli.

Taarifa kutoka tovuti ya The Athletic inaeleza dizaini hiyo iliyobuniwa na Sir Norman Foster kisha kupitishwa na tajiri Sir Jim Ratcliffe, ilikuwa na lengo la kuwalinda mashabiki dhidi ya mvua na upepo, pia kubadilisha taswira ya dimba la Old Trafford kuwa uwanja wa kipekee duniani.

Hata hivyo, mazungumzo ya ununuzi wa ardhi iliyohitajika ili kuwezesha mpango wa kujenga paa hilo yamegonga mwamba.

Kampuni ya usafirishaji Freightliner ambayo inamiliki sehemu kubwa ya ardhi magharibi mwa Old Trafford, eneo ambalo United iliihitaji kwa ajili ya ujenzi wa uwanja mpya inaelezwa inataka pesa nyingi kuliko kiasi ambacho Man United ilipanga kutoa.

Freightliner inahitaji Pauni 400 milioni, mara nane zaidi ya makisio ya Man United ambayo ilikuwa na matumaini ya kununua eneo hilo kwa Pauni 50 milioni pekee.

Kampuni hiyo ambayo kwa sasa inatumia eneo hilo kama sehemu ya kuhifadhi baadhi ya mzigo yake, imeiambia Man United kwamba itakubali kuuza sehemu hiyo kama tu italipwa kiasi hicho.

Kutokana na hali hiyo, Man United inalazimika kufikiria upya mradi mzima, kuanzia michoro na bajeti kwa ujumla.

Ramani ya awali ilionekana kuvutia watu wengi na Machi mwaka huu ilipoonyeshwa, tajiri Ratcliffe ambaye ndio anataka kujenga uwanja, alitangaza kwamba uwanja huo mpya utakuwa “alama ya dunia” na jengo ambalo kila mtu atakapoliona, atakubali na kulisifia.