Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man United ilivyomkosa Donnarumma

MAN Pict

Muktasari:

  • Hata hivyo, usajili wa kipa huyo ulishangaza wengi kwani walidhani angesajiliwa Gianluig Donnarumma kutoka Paris Saint-Germain ambaye alionekana mbadalala sahihi wa Onana kutokana na uzoefu na kiwango ambacho amekionyesha akiwa na miamba hiyo ya Ufaransa na timu ya taifa ya Italia.

MANCHESTER, ENGLAND: Dirisha lililopita la usajili wa majira ya kiangazi, Manchester United ilikuwa miongoni mwa timu za mwisho kufanya usajili na ilimtoa kwa mkopo Andre Onana kwenda Trabzanspor kisha ikamsajili Senne Lammens kutoka Royal Antwerp ya Ubelgiji.

Hata hivyo, usajili wa kipa huyo ulishangaza wengi kwani walidhani angesajiliwa Gianluig Donnarumma kutoka Paris Saint-Germain ambaye alionekana mbadalala sahihi wa Onana kutokana na uzoefu na kiwango ambacho amekionyesha akiwa na miamba hiyo ya Ufaransa na timu ya taifa ya Italia.

Ripoti mpya kutoka tovuti ya The Telegraph imefichua sababu kubwa iliyoifanya Man United iachane na mpango wa kumsajili kipa huyu na Emiliano Martinez kutoka Aston Villa ilikuwa ni pesa.

Ripoti hiyo inaeleza Man United iliambiwa ingelazimika kulipa ada ya uhamisho ya Pauni 35 milioni na kutoa mshahara wa mwaka wa Pauni 17.4 milioni ambayo ni takriban Pauni 330,000 kwa wiki ili kumpata kipa huyo.

Kiasi cha pesa cha ada ya uhamisho pamoja na mshahara kingeigharimu Man United takribani Pauni 120 hadi 140 milioni kwa sababu ilitaka kumsainisha mkataba wa miaka mitano hadi sita.

Baada ya Man United kuachana na mpango huo, Donnarumma alijiunga na Manchester City ambayo ililipa Pauni 26 milioni kama ada ya uhamisho na kumsainisha mkataba wa miaka mitano.

Ripoti pia inaeleza Man United ilihitaji kumsajili kipa wa Aston Villa, Emiliano Martínez, lakini ada ya Pauni 30 milioni na mshahara wa kila mwaka wa Pauni 10 milioni pia ilionekana kuwa kubwa mno.

Hivyo, klabu iliamua kumchagua Lammens mwenye umri wa miaka 23 ambaye, licha ya kwamba haokani kuonyesha makali sana aliwagharimu Pauni 18.2 milioni tu.