Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man United? Sijui itakuwaje sasa

MAN Utd Pict

Muktasari:

  • Kwa kipigo hicho kutoka kwa Fulham, hiyo ina maana taji pekee lililobaki kwa Man United ni Europa League na bingwa anapata tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

MANCHESTER, ENGLAND: KUTUPWA nje kwa mikwaju ya penalti na Fulham Kombe la FA kuna madhara makubwa kwa Manchester United wakati huu ikipita kwenye majanga makubwa na kujiweka mbali na ndoto za kubeba walau taji moja la kujifariji msimu huu.

Kwa kipigo hicho kutoka kwa Fulham, hiyo ina maana taji pekee lililobaki kwa Man United ni Europa League na bingwa anapata tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Kushindwa kubeba ubingwa wa Europa League hilo litafanya Man United kutocheza kwenye michuano yoyote ya Ulaya msimu ujao na itakuwa mara yao ya pili kwenye kipindi cha miongo mitatu iliyopita.

Kwa kiwango cha sasa cha Man United kuna uwezekano mgumu wa kunyakua ubingwa wa Europa League na hilo likitokea, basi timu hiyo haitakuwa na mvuto kwa wachezaji dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi. 

Kwa kuzingatia tatizo la kifedha la Man United, ambayo imeripoti hasara ya Pauni 300 milioni kwa miaka mitatu iliyopita watahitaji kutumia akili nyingi sana kwenye usajili wa dirisha lijalo na kuachana na namna ambayo ilikuwa ikifanya huko nyuma.

Tatizo la kiuchumi limefanya Man United kupunguza wafanyakazi 250 na bado kuna 200 wengine watapunguzwa pia ili kuwa na bajeti itakayowafanya wasajili dirisha lijalo. 

Man United inahitaji pia kuuza wachezaji ili isajili upya, lakini kama itashindwa kukamatia tiketi ya kucheza michuano ya Ulaya, itawaweka kwenye wakati mgumu kunasa mastaa wa maana.

Kinara wa muda wa mabao wa Man United na nahodha wa zamani wa kikosi hicho cha Old Trafford, Wayne Rooney, aliweka wasiwasi juu ya mwenendo wa timu hiyo kama wataweza kusajili wachezaji wa viwango vikubwa, aliposema: “Kama ningekuwa mchezaji mkubwa nacheza kwenye nchi nyingine na Manchester United inakuja kunisajili kwa sasa, ningesema 'sina uhakika'.”

“United imetumia pesa nyingi sana kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita. Hakuwa na mfumo, kwa sababu kocha hakuwa anapewa muda mwingi. Kila wakati wanapoonekana wanasoka mbele, wanatibua na kuingia kwenye staili tofauti.”

Kama Man United itashindwa kunasa tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao, isahau ishu ya kusajili mastaa wa maana kama straika wa Sporting Lisbon, Viktor Gyokeres, wa Napoli, Victor Osimhen au mkali wa Wolves, Matheus Cunha. 

Man United inafahamu wazi nguvu yao kwa sasa imepungua baada ya kuwakosa mastaa wa maana kabisa kama Erling Haaland na Jude Bellingham na wote hao Kocha Ole Gunnar Solskajer alijaribu kuwasajili na kushindwa kuwanasa. Haaland alijiunga na Manchester City na Bellingham alitimkia zake Borussia Dortmund kabla ya sasa kutamba na Real Madrid kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.