Man United kujiuliza leo

Man United kujiuliza leo

Muktasari:

Manchester United imekuwa kwenye hali mbaya kwenye Ligi Kuu kwa  msimu huu, ambapo inashika nafasi ya tisa ikiwa imecheza mechi tisa, ikishinda tano, sare moja na imefungwa tatu

MANCHESTER, ENGLAND
BAADA ya kupoteza mchezo wa hatua ya makundi wa michuano ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya PSG mapema wiki hii, Manchester United leo itashuka dimbani kujiuliza kwenye muendelezo wa Ligi Kuu England dhidi ya West Ham United.
Man United inaingia kwenye mchezo huo utakaopigwa katika dimba la London Stadium, majira ya 2:30 usiku, ikiwa na kumbu kumbu mbaya ya kupoteza mchezo wa PSG na inakutana na West Ham ambayo ipo kwenye kiwango kizuri kwa sasa ikiwa inashika nafasi ya tano kwa alama 17.
Mchezo wa mapema utakuwa kati ya Burnley na Everton utakaopigwa saa 9:30 mchana. Huku Manchester City inayoshika nafasi ya 11 na pointi zake 15 itaumana na Fulham inayoshikilia nafasi ya 17, mchezo huo utapigwa majira ya 12:00 jioni.
Wababe wa London, Chelsea iliyo nafasi ya tatu itaialika Leeds United kwenye mchezo wa mwisho kwa  leo utakaopigwa saa 5:00 jioni.
Huko Hispania, Levante itaialika Getafe katika mechi itakayopigwa saa 10:00 jioni, huku Sevilla
 itakuwa na kazi ya kuivimbia Real Madrid iliyo kwenye hali mbaya, mechi itachezwa saa 12:15 jioni na 
Atletico Madrid itapepetana na Real Valladolid saa 2:30 usiku. Mchezo wa mwisho utakuwa kati ya Cadiz na Barcelona saa 5:00 usiku.
Vile vile huko Ujerumani kwenye Bundesliga FC Koln itaialika Wolfsburg,  Arminia Bielefeld
itacheza na Mainz 05 huku Eintracht Frankfurt itakuwa na kibarua kizito mbele ya Borussia Dortmund na Freiburg itajipima ubavu na Borussia Moenchengladbach.
Mchezo wa kukata na shoka utakuwa kati ya wababe wa ligi hiyo Bayern Munich itakayoialika kwenye dimba la Allianz Arena na mchezo utapigwa saa 2:30 usiku.