Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man United, Chelsea mambo magumu kwa Sesko

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Timu mbalimbali ikiwamo Chelsea na Manchester United ambazo zilikuwa zikihitaji huduma ya fundi huyu zimeonekana kurudi nyuma kutokana na kiasi hicho cha pesa kinachohitajika na Leipzig ambao licha ya kuzungumza nao wamekataa kupunguza bei.

MABOSI wa RB Leipzig wameendelea kushikilia msimamo wao wa kuhitaji euro 100 milioni ili kumuuza mshambuliaji wa kimataifa wa Slovakia, Benjamin Sesko, 22, katika dirisha hili.

Timu mbalimbali ikiwamo Chelsea na Manchester United ambazo zilikuwa zikihitaji huduma ya fundi huyu zimeonekana kurudi nyuma kutokana na kiasi hicho cha pesa kinachohitajika na Leipzig ambao licha ya kuzungumza nao wamekataa kupunguza bei.

Mkataba wa staa huyu unatarajiwa kumalizika mwaka 2029, msimu uliopita alicheza mechi 45 za michuano yote na kufunga mabao 21.

Kwa mujibu wa watu wake wa karibu ni kwamba staa huyu yupo tayari kuondoka lakini hatalazimisha kufanya hivyo, ikiwa timu zinazomhitaji hazitafikia mwafaka na Leipzig.

Mchezaji huyo pia amezivutia klabu vikubwa kama Manchester United, Manchester City, na Real Madrid, kama ilivyoripotiwa awali na CaughtOffside.

Christian Falk, kwa upande mwingine, hivi karibuni aliweka wazi kuwa Sesko alipokea ofa kutoka Ligi Kuu ya Saudi Arabia, lakini kocha wa timu ya taifa lake alimshauri asihamie huko kwa sasa.

Ilithibitishwa kuwa Manchester United inamfuatilia Sesko kwa karibu, jambo linalopunguza vita ya kumhitaji sokoni, hasa kwa kuwa Arsenal sasa imehamishia nguvu zake kwa Viktor Gyokeres.

United inahitaji mshambuliaji katika dirisha hili la majira ya joto, na kwa mujibu wa The Athletic, pia imemtaja mshambuliaji wa Aston Villa, Ollie Watkins, kama mmoja wa inaowafikiria, huku mazungumzo ya awali yakiwa yamefanyika.


Noni Madueke

CHELSEA inatarajia kupokea ofa inayofikia pauni 50 milioni kutoka Arsenal kama ada ya uhamisho ya kuwauzia winga wao raia wa England mwenye umri wa miaka 23, Noni Madueke, ambaye tayari amekubali kujiunga na washika mitutu hao wa Jiji la London.

Mkataba wa Madueke unatarajiwa kumalizika mwaka 2030.


Mohammed Kudus

TOTTENHAM bado ziko kwenye mazungumzo na West Ham kuhusu kiungo wa kulia wa timu hiyo na Ghana, Mohammed Kudus, kwa ajili ya kuipata saini yake katika dirisha hili la majira ya kiangazi.

Awali, West Ham ilidaiwa kukataa ofa ya karibia pauni 50 milioni kutoka kwa Spurs kwa ajili ya kiungo huyo ambaye mkataba wake unamalizika mwaka 2028.


Warren Zaire-Emery

MABOSI wa Manchester United wametuma wawakilishi wao kwenda Ufaransa kufanya kuzungumza na Paris St-Germain kwa ajili ya kumsajili kiungo wa timu hiyo na Ufaransa, Warren Zaire-Emery, 19, katika dirisha hili la majira ya kiangazi.

Staa huyu amekuwa akifuatiliwa na Man United kwa muda sasa akiwa na PSG na timu ya taifa.


Josh Sargent

BURNLEY imeendelea kushikilia msimamo wake wa kuhitaji pauni 50 milioni ili kumuuza beki wa kati raia wa Ufaransa, Maxime Esteve, 23, ambaye anawindwa sana na  Bayern Munich.

Inaelezwa kocha wa Bayern, Vincent Kompany ni shabiki mkubwa wa staa huyu ambaye aliwahi kumfundisha staa akiwa Burnley.


Chukwuemeka

BORUSSIA Dortmund inataka kumuongeza mkataba mwingine wa mkopo kiungo wa Chelsea, Carney Chukwuemeka, 21, ili kuendelea kumtumia kwa msimu ujao.

Awali, mabosi wa Dortmund walikuwa tayari kumsainisha mkataba wa kudumu lakini wameshindwa kufanya hivyo kutokana na kiasi kikubwa cha pauni 40 milioni kinachohitajika na Chelsea kama ada yake ya uhamisho.


Borna Sosa

CRYSTAL Palace iko katika hatua za mwisho kukamilisha usajili wa beki wa kushoto wa Ajax mwenye umri wa miaka 27, Borna Sosa, kwa pauni  2 milioni katika dirisha hili.

Palace inataka kusuka upya kikosi chake baada ya kuuza wachezaji kadhaa katika dirisha hili.

Mkataba wa Sosa unatarajiwa kumalizika mwaka 2028.


Junior Firpo

REAL Betis imewasilisha ofa ya mkataba wa miaka mitatu kwa beki wa zamani wa Leeds United, Junior Firpo, mwenye umri wa miaka 28, ambaye ameachana na timu yake mwisho wa msimu uliopita.

Licha ya kupokea ofa hiyo, staa huyu wa kimataifa wa Jamhuri ya Dominika hadi sasa bado hajafanya uamuzi kama atajiunga nao au laa.