Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man united bana mshahara tembo, matokeo sisimizi

LONDON, ENGLAND. WAKATI mwingine, pesa si kila kitu. Ndiyo hivyo.

Manchester United bili yao ya mishahara ni zaidi ya mara 50 ya kile kinacholipwa na Luton Town kwa wachezaji wao kwenye Ligi Kuu England msimu wa 2023-24.

Lakini, nenda kwenye matokeo yao ya uwanjani, katika mechi tano ilizocheza Man United kwenye Ligi Kuu England msimu huu, wamechapwa tatu.

Kuhusu mshahara, staa wa Manchester City, Kevin De Bruyne, peke yake analipwa mara nne zaidi ya kikosi kizima cha Luton.

Lakini, kumekuwa na sapraizi chache linapokuja suala la bili za mishahara inayolipwa kwenye Ligi Kuu England msimu huu wa 2023-24.

Man United ndiyo timu inayolipa mshahara mkubwa zaidi baada ya kuwaongeza wakali Andre Onana, Mason Mount na Rasmus Hojlund kwenye bili yao ya mishahara, huku ikimpa dili tamu zaidi mshambuliaji wao Marcus Rashford.

Hata hivyo, mshahara huo wa Man United kwa msimu huu umepungua kwa kiasi kikubwa baada ya kuachana na mastaa Cristiano Ronaldo na David de Gea, waliokuwa wakilipwa mishahara mikubwa zaidi kwenye kikosi hicho.

Mabingwa watetezi, Manchester City nao hawajaachwa mbali sana kwenye kulipa mishahara mikubwa. Lakini, miamba hiyo inayonolewa na Pep Guardiola mambo yao ya uwanjani yapo vizuri, yanaendana na mshahara unaolipwa. Man City imevuka bili ya Pauni 200 milioni kwa mwaka huku wakali De Bruyne na Erling Haaland wakiongoza kwa kulipwa mishahara mikubwa huko Etihad.

Arsenal wanakuja juu, kwa sasa wanashika nafasi ya tatu kwenye chati ya bili ya mishahara baada ya kufanya usajili wa mastaa kadhaa kwenye dirisha lililopita la uhamisho wa majira ya kiangazi baada ya kurejea kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya kwanza tangu 2016.

Chelsea hawamo kwenye michuano yoyote ya Ulaya msimu huu wa 2023-24, hivyo bili yao ya mishahara ya Pauni 128 milioni wanayolipa kwa mwaka inaonekana kuwa ni matumizi ya hovyo ya pesa.

Bilionea mmiliki wa klabu hiyo ya Stamford Bridge, Todd Boehly amekuwa gumzo baada ya kuleta mastaa kibao, lakini akiwafungulia mlango wa kutokea mastaa waliokuwa wakilipwa pesa nyingi kama N’Golo Kante, Mason Mount, Kalidou Koulibaly, Mateo Kovacic, Kai Havertz, Christian Pulisic, Pierre-Emerick Aubameyang na nahodha Cesar Azpilicueta.

Miaka ya nyuma Liverpool walikuwa wakidaiwa kuwa wagumu kwenye mambo ya usajili, lakini miaka ya karibuni, kocha Jurgen Klopp amefungulia pochi na kulipa mastaa wake mishahara minono. Kwenye kikosi hicho kuna mastaa wanaolipwa pesa ndefu kama Mohamed Salah na Virgil van Dijk.

Hata hivyo, kwenye dirisha lililopita la uhamisho wa majira ya kiangazi, Liverpool imeachana na mastaa wake kadhaa akiwamo Jordan Henderson, James Milner, Fabinho, Alex Oxlade-Chamberlain, Naby Keita na Roberto Firmino na hivyo kuwapunguzia bili yao ya mishahara.

Tottenham Hotspur imeondoka kwenye orodha ya timu sita za juu baada ya kuachana na straika wao namba moja, Harry Kane, huko Aston Villa wakipanda hadi kwenye namba sita.

Everton bado wapo kwenye orodha ya timu zenye bili kubwa za mishahara, ikishika namba 10, lakini matokeo yao ya ndani ya uwanja bado kuna tatizo. Nottingham Forest nao mambo yao si mabaya kwenye ishu ya kulipa mishahara, huku Newcastle United wakishika namba nane, nyuma ya West Ham United.

Brighton, waliokuwa namba sita msimu uliopita na Brentford wa tisa, wanatajwa kama moja ya timu zilizopiga hatua kubwa kwenye Ligi Kuu England miaka ya karibuni. Miamba hiyo bili yao ya mishahara ni Pauni 47 milioni na Pauni 34 milioni mtawalia.

Chini kabisa, timu tatu zilizopanda daraja msimu huu, ndizo zenye bili ndogo ya mishahara, lakini kikosi cha Vincent Kompany, Burnley kinalipa zaidi ya mara sita ya mshahara unaolipwa huko Luton kwa mwaka.

Kwa mujibu wa FBref kwa kupitia Capology, hii hapa mishahara inayolipwa kwa mwaka kwa kila timu kwenye Ligi Kuu England msimu huu.