Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man City yamponza aguero, aliwa Sh 26M

Muktasari:

  • Mabingwa hao wa Ligi Kuu England waliikaribisha miamba hiyo ya Hispania kwenye Uwanja wa Etihad kwa ajili ya mechi hiyo ya kwanza ya mchujo wa kuwania tiketi ya kucheza mtoano wa hatua ya 16 bora kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.

MANCHESTER, ENGLAND: STAA wa soka, Sergio Aguero amelazimika kuangua kicheko cha aibu baada ya kuahidi kwamba atakata korodani zake endapo kama Manchester City itapoteza mbele ya Real Madrid katika mchzo wa kwanza wa mchujo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya uliofanyika usiku wa juzi Jumanne huko Etihad.

Mabingwa hao wa Ligi Kuu England waliikaribisha miamba hiyo ya Hispania kwenye Uwanja wa Etihad kwa ajili ya mechi hiyo ya kwanza ya mchujo wa kuwania tiketi ya kucheza mtoano wa hatua ya 16 bora kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Na kilichotokea kwenye mchezo huo, Man City ilikubali kichapo cha mabao 3-2 licha ya kutangulia mara mbili kwa mabao ya straika Erling Haaland.

Haaland alitangulia kufunga kabla ya Kylian Mbappe kusawazisha. Man City ilitangulia tena kwa bao la mkwaju wa penalti iliyopigwa na Haaland, lakini mchezaji wa zamani wa Man City, Brahim Diaz alisawazishia Real Madrid kabla ya Jude Bellingham kufunga la ushindi kwa Los Blancos dakika za majeruhi.

Wakati kipigo hicho kikiwa na maumivu kwa Man City, mambo yatakuwa machungu zaidi kwa straika wa zamani wa miamba hiyo, Aguero, ambaye alitoa ahadi kabla ya mechi hiyo, aliposema: "Real Madrid haiwezi kuifunga Man City. Kama wataifunga City, nitakata korodani zangu."

Aguero alibeti pia Dola 10,000 (Sh 25,752,100) kwamba yatafungwa mabao mawili kipindi cha kwanza, pesa ambayo ililiwa kwa kuwa kipindi cha kwanza, mechi hiyo ilishuhudia bao moja tu lililofungwa na Haaland.

Mmoja wa wapinzani wa Aguero wa zamani, Wayne Rooney alisema Man City inaelekea kubaya baada ya kudai kwamba wachezaji wa kikosi hicho kinachonolewa na Pep Guardiola waliingia kwenye huku ikiwa kama hawaaminiani, ambapo staa huyo wa zamani wa Manchester United alisema: "Kulikuwa na ujinga mwingi kwa wachezaji wa Man City, hasa kwenye dakika za mwisho za mchezo. Wachezaji walionekana kama hawaaminiani hivi na hilo litamshtua Guardiola."

Aguero sasa atalazimika tu kuwa mpole akisubiri mechi ya marudiano itakayopigwa Hispania wiki ijayo. Kwenye mchezo huo, Man City italazimika kushinda ili kupata tiketi hiyo ya kuingia kwenye hatua ya 16 bora.

Kama itashindwa kufanya hivyo, basi itakuwa mara yao ya kwanza kutolewa mapema kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya tangu msimu wa 2012/13, walipokomea kwenye hatua ya makundi - kitu kinachofanana na msimu huu baada ya michuano hiyo kubadilishwa na kuwa kwenye mtindo tofauti.

Kabla ya kwenda kurudiana na Real Madrid, Man City itakuwa na mtihani mwingine kwenye kurudi kwenye ubora wao huko kwenye Ligi Kuu England.

Kikosi hicho cha Guardiola kitakuwa nyumbani kukipiga na Newcastle United wikiendi hii, wakisaka ushindi ili kurudi kwenye Top Four.


TAKWIMU ZA MCHEZO MAN CITY vs REAL MADRID

-Mashuti golini: Man City 4, Real Madrid 8

-Mashuti yote: Man City 11, Real Madrid 20

-Mashuti kuzuiwa: Man City 4, Real Madrid 5

-Umiliki mpira: Man City 54%, Real Madrid 46%

-Pasi zilizopigwa: Man City 497, Real Madrid 420

-Pasi sahihi: Man City 450, Real Madrid 376

-Kona zilizopigwa: Man City 6, Real Madrid 5