Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man City Liverpool hii usicheze mbali inatoa 1.5 mwanangu

Muktasari:

  • Kwenye upande wa kufungwa, Liverpool imeruhusu nyavu zao kutikiswa mara 26, Man City mara 35.

MANCHESTER, ENGLAND: LIVERPOOL imetikisa nyavu mara 62 kwenye Ligi Kuu England hadi sasa. Manchester City yenyewe imetupia kwenye nyavu za wapinzani mara 52. Kwa pamoja timu hizo zimefunga mabao 114.

Kwenye upande wa kufungwa, Liverpool imeruhusu nyavu zao kutikiswa mara 26, Man City mara 35.

Hiyo ina maana, timu hizo nyavu zao zimeguswa mara 61. Kwa maana hiyo, timu hizo zinafunga, lakini pia zinafungika. Na leo, Jumapili zinakutana zenyewe huko Etihad kwenye mchezo wa Ligi Kuu England.

Kwa namba hizo, ukiweka ile 1.5 inatoa bila shida kabisa. Hata 2.5 haiwezi kukusaliti kwa fowadi ya timu hizo zilivyokuwa bize kutumbukiza mipira nyavuni, huku mabeki nao wakiwa wanashindwa kabisa kukaba.

Kinara wa mabao kwenye Ligi Kuu England ni Mohamed Salah, ambaye ametikisa nyavu mara 24. Huyo ni staa wa Liverpool, hivyo atakuwapo uwanjani kwenye mchezo huo wa Etihad.

Anayeshika namba mbili kwa mabao kwenye ligi hiyo msimu huu ni Erling Haaland wa Man City, ametikisa nyavu mara 19. Hadi hapo, unaweza kuona mechi hiyo inavyokwenda kuwa ya mabao.

Mechi tano za mwisho zilizokutanisha timu hizo kwenye Ligi Kuu England, mabao 12. Na katika mechi hizo ni moja tu, ndiyo ambayo ilishindwa kutoa 1.5 kwa maana ya mabao mawili kwenda mbele ni ile ya ushindi wa bao 1-0 iliyopata Liverpool uwanjani Anfield, Oktoba 16, 2022.

Kwenye mechi za Ligi Kuu England, Man City na Liverpool zimekutana mara 55, ambapo katika mara 21 ilikuwa sare, huku vijana wa Pep Guardiola, Man City wakiibuka na ushindi kwenye mechi 12, mara 10 nyumbani na mbili tu ugenini, wakati jeshi la Arne Slot,  Liverpool limeshinda 22, mara 18 nyumbani na nne ugenini. Safari hii itakuwaje? Ngoja tuone, ambapo Liverpool inasaka ubingwa na Man City inataka Top Four.

Mechi nyingine ya Ligi Kuu England itakayopigwa leo, Newcastle United itakuwa nyumbani kukipiga na Nottingham Forest katika mechi inayotarajiwa kuwa na upinzani mkali ndani ya uwanja.