Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mambo ni moto njia ya ubingwa Kombe la Dunia

Muktasari:

  • Kikosi hicho cha kocha Thomas Tuchel kwenye kundi lake imepangwa kuanza kucheza na Croatia, Ghana na kisha Panama. Na kwenye kundi hilo, England inapewa nafasi ya kuongoza na kushika namba moja.

LONDON, ENGLAND: ENGLAND itaomba kumaliza nafasi ya pili kwenye kundi lao la Kombe la Dunia 2026 ili kuwa na nafasi ya kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kwenda kunyakua ubingwa huo.

Kikosi hicho cha kocha Thomas Tuchel kwenye kundi lake imepangwa kuanza kucheza na Croatia, Ghana na kisha Panama. Na kwenye kundi hilo, England inapewa nafasi ya kuongoza na kushika namba moja.

England ilimaliza nafasi ya pili kwenye kundi lake wakati wa fainali za Kombe la Dunia 2018, lakini ilipata njia nzuri, ikiwamo kukabiliana na Sweden kwenye hatua ya robo fainali.

Lakini, kwenye fainali za Kombe la Dunia 2026, endapo itamaliza nafasi ya kwanza kwenye kundi lake itakuwa na nafasi ya kukabiliana na timu itakayokuwa imemaliza nafasi ya tatu bora kwenye kundi, inaweza kuwa moja kati ya timu hizo, Ivory Coast, Saudi Arabia, Senegal, Algeria na Uzbekistan kwenye hatua ya 32 bora.

Wenyeji wenza, Mexico wanaweza kuja kukabiliana na England kwenye hatua ya 16 kitu ambacho kinaelezwa kinaweza kuwa kigumu kwa kikosi cha Three Lions. Ikipenya kwenye hatua hiyo, inaweza kwenda kukabiliana na Brazil katika robo fainali, ikiwa mpinzani ambaye England haijawahi kupata ushindi dhidi yao katika mechi za kiushindani.

Na kama itapenya hapo, kuna uwezekano wa kwenda kuwakabili Argentina katika hatua ya nusu fainali kabla ya kufikia fainali.

Endapo kama itamaliza nafasi ya pili, njia yao ya kuelekea kwenye ubingwa haitakuwa ngumu. Hilo likitokea, England itazikwepa Hispania, Argentina na Ufaransa hadi hapo itakapofika hatua ya nusu fainali.

Kwenye raundi ya 32 bora, England inaweza kucheza na timu itakayokuwa imemaliza nafasi ya pili kwenye Kundi K ambalo baadhi ya timu zake ni Ureno na Colombia. Kwenye robo fainali inaweza kucheza na Ubelgiji, kisha Ufaransa kwenye nusu fainali na fainali inaweza kuwa na Argentina.

England inapambana kusaka taji lake la kwanza la Kombe la Dunia, ambako kwa mara ya mwisho ililibeba miaka 60 iliyopita huku kocha Thomas Tuchel akiwa na matumaini makubwa ya kuipa nchi hiyo taji kubwa kabisa la kisoka.


MAKUNDI YA KOMBE LA DUNIA 2026

Kundi A: Mexico, Afrika Kusini, Korea Kusini, Winner playoff D

Kundi B: Canada, Winner playoff A, Qatar, Switzerland

Kundi C: Brazil, Morocco, Haiti, Scotland

Kundi D: Marekani, Paraguay, Australia, Winner playoff C

Kundi E: Ujerumani, Curacao, Ivory Coast, Ecuador

Kundi F: Uholanzi, Japan, Winner playoff B, Tunisia

Kundi G: Ubelgiji, Misri, Iran, New Zealand

Kundi H: Hispania, Cape Verde, Saudi Arabia, Uruguay

Kundi I: Ufaransa, Senegal, Winner playoff 2, Norway

Kundi J: Argentina, Algeria, Austria, Jordan

Kundi K: Ureno, Winner playoff 1, Uzbekistan, Colombia

Kundi L: England, Croatia, Ghana, Panama.