Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kurudi Anfield... Klopp asema kitu!

KLOP Pict

Muktasari:

  • Kocha huyo mwenye hadhi kubwa huko Anfield kwa sasa ni bosi wa soka kwenye klabu za Red Bull's na hivi karibuni alitangazwa kuunda jopo la kusaidia Ligi ya Soka ya Ujerumani (DFL) kupandisha viwango na kukuza vipaji vipya.

LIVERPOOL, ENGLAND: KOCHA, Jurgen Klopp amefunguka juu ya uwezekano wa kurejea kuinoa Liverpool akidai hilo kinadharia inawezekana.

Kocha huyo mwenye hadhi kubwa huko Anfield kwa sasa ni bosi wa soka kwenye klabu za Red Bull's na hivi karibuni alitangazwa kuunda jopo la kusaidia Ligi ya Soka ya Ujerumani (DFL) kupandisha viwango na kukuza vipaji vipya.

Januari 2024, Klopp alibainisha kwenye mahojiano yaliyojaa hisia kubwa kwamba ataachana na Liverpool mwishoni mwa msimu wa 2023-24. Aliondoka Anfield akiwa ameshinda Ligi Kuu England, Ligi ya Mabingwa Ulaya, Kombe la FA, Kombe la Ligi mara mbili na Kombe la Dunia la Klabu. Alipozungumza katika kipindi cha redio mtandao cha Diary of a CEO, Klopp, wakati alipoulizwa kama atarudi Liverpool, alijibu: "Nilisema kwamba sitakwenda kuwa kocha wa timu tofauti England. Hivyo, kama nitarudi England, basi itakuwa Liverpool. Ndiyo, kinadharia inawezekana."

Alipoulizwa ni kitu gani kifanyike ili kumfanya arudi Anfield, alijibu: "Sifahamu hakika. Napenda ninachokifanya. Sijamisi kufundisha. Nafanya ukocha, lakini kwenye njia tofauti, sio wachezaji.

KLO 02

"Sijamisi. Sijamisi kusimama kwenye mvua kwa saa mbili na nusu hadi tatu. Na sijamisi pia kwenda kwenye mikutano ya vyombo vya habari mara tatu kwa wiki.

"Kufanyiwa mahojiano mara 10 au 12 kwa wiki, sijamisi bado hivyo vitu. Sijamisi kuwa kwenye vyumba vya kubadilishia. Nilikuwa kocha kwenye mechi karibu 1,080 na nimekuwa kwenye vyumba vya kubadilishia mara nyingi sana.

"Sitaki kufa nikiwa kwenye vyumba vya kubadilishia. Ipo hivyo. Nina miaka 58, kwenye eneo hilo naweza kuonekana ni mzee, lakini kwenye maeneo mengine bado sijawa mzee.

"Hii ina maana nitafanya uamuzi miaka michache ijayo. Sijui kwa sasa. Nikisema leo, nitakwambia sitakuwa kuwa kocha tena, lakini namshukuru Mungu siwezi kuamua hilo leo, acha tusubiri tuone ni kitu gani kitatokea huko baadaye."

Kisha Klopp alizungumzia wadhifa wake kwenye klabu za Red Bull akisema: "Kwa sasa nafanya mradi ninaoupenda na kushirikiana na watu vizuri kabisa. Napenda ninachokifanya kwa sasa.”

KLO 01

Liverpool ilifanikiwa kushinda ubingwa wa Ligi Kuu England baada ya kuwa chini ya Arne Slot, kocha aliyerithi mikoba ya Klopp msimu uliopita. Lakini, kwa siku za hivi karibuni, timu hiyo ambayo inatajwa kama moja ya zile zinazokimbizia ubingwa, imepoteza mechi tatu mfululizo kwenye Ligi Kuu England dhidi ya Crystal Palace, Chelsea na Manchester United uwanjani Anfield zilipokutana Jumapili iliyopita.