Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Makundi ya mtego, visasi Kombe la Dunia

Muktasari:

  • Ni droo iliyotengeneza mechi zenye mvuto kwa makundi mengi kwa kukutanisha timu nyingi ambazo ziliwahi kukutana kwenye mashindano hayo hapo nyuma, jambo linaloweza kuzifanya mechi za mwakani zionekane kama za kulipa kisasi kwa baadhi ya timu au nyingine kuendeleza ubabe kutegemeana na matokeo ya nyuma baina yao.

Makundi ya Fainali za Kombe la Dunia 2026 yamejulikana rasmi, Ijumaa, Desemba 5, 2025 baada ya kukamilika kwa droo ya upangaji wake iliyofanyika huko Washington DC, Marekani.

Ni droo iliyotengeneza mechi zenye mvuto kwa makundi mengi kwa kukutanisha timu nyingi ambazo ziliwahi kukutana kwenye mashindano hayo hapo nyuma, jambo linaloweza kuzifanya mechi za mwakani zionekane kama za kulipa kisasi kwa baadhi ya timu au nyingine kuendeleza ubabe kutegemeana na matokeo ya nyuma baina yao.

Wawakilishi wa Afrika na timu pekee kutoka Kanda ya Kusini mwa Afrika, Afrika Kusini ‘Bafana Bafana’ wamepangwa katika kundi ambalo lina wenyeji Mexico, Korea Kusini na timu mojawapo itakayofuzu kupitia mchujo kati ya Denmark, Jamhuri ya Czech, Jamhuri ya Ireland au Macedonia Kaskazini.

Kutakuwa na marudio ya nusu fainali ya Kombe la Dunia 2018 baina ya Croatia na England kwa vile timu hizo zimepangwa kundi moja ambalo ni L likiwa pia na Panama na Ghana.

Kama England itasonga mbele hadi robo fainali na Brazil ikafanya hivyo, timu hizo zinaweza kukutana katika hatua ya robo fainali ya mashindano hayo.

Brazil imepangwa katika kundi C lenye Morocco, Scotland na Haiti.

Kitendo cha Senegal kupangwa kundi I pamoja na Ufaransa hapana shaka kunafanya mechi baina yao kukumbushia mchezo wa ufunguzi wa Kombe la Dunia 2002 ambao Senegal iliichapa Ufaransa kwa bao 1-0.

Katika kundi hilo I, Ufaransa na Senegal zitakuwa pia na timu za Norway na timu moja itakayopita katika mechi za mchujo wa mabara.

Ivory Coast ambayo mwakani itashiriki Fainali za Kombe la Dunia kwa mara ya nne, imeangukia katika kundi E lenye Ujerumani, Ecuador na Curacao.

Mabingwa watetezi wa Kombe la Dunia, Argentina wao wamepangwa kundi J wakiwa na timu za Austria, Algeria na Jordan.

Wakishiriki kwa mara ya kwanza Fainali za Kombe la Dunia, Cape Verde wamepangwa katika kundi H lenye timu za Hispania, Uruguay na Saudi Arabia.