Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Makocha saba mlangoni Spurs

Muktasari:

  • Tudor mwenye miaka 47 aliletwa kwa kazi moja kuzuia mfululizo wa matokeo mabaya ili kuiokoa Spurs. Lakini, kushindwa mechi nne huku wakiruhusu mabao 14 kumefanya timu hiyo ya London kubaki pointi moja tu juu ya eneo la kushuka daraja, huku pia wakikaribia kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.

LONDON, ENGLAND: MAMBO si shwari. Tottenham Hotspur imendelea kuzorota chini ya kocha Igor Tudor. Kipigo cha aibu cha mabao 5-2 ilichopata kutoka kwa Atletico Madrid usiku wa Jumanne kilikuwa cha nne mfululizo kupoteza tangu Tudor alipochukua mikoba ya kuinoa timu hiyo.

Tudor mwenye miaka 47 aliletwa kwa kazi moja kuzuia mfululizo wa matokeo mabaya ili kuiokoa Spurs. Lakini, kushindwa mechi nne huku wakiruhusu mabao 14 kumefanya timu hiyo ya London kubaki pointi moja tu juu ya eneo la kushuka daraja, huku pia wakikaribia kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Uamuzi wote wa Tudor umeonekana kwenda vibaya kabisa kuanzia kumtumia Conor Gallagher kama winga dhidi ya Fulham, kumchezesha Pedro Porro kama beki wa kati dhidi ya Crystal Palace, hadi uamuzi wa kumuacha benchi kipa Guglielmo Vicario na kumpa nafasi Antonín Kinský dhidi ya Atlético kabla ya kumtoa mapema tu kipindi cha kwanza.

Uhalisia ni kwamba Tudor yuko karibu kufukuzwa kazi siku 25 tu baada ya kuchukua nafasi ya Thomas Frank. Lakini, swali ni nani atakuja kuchukua mikoba yake? Hapa chini ni baadhi ya makocha wanaoweza kuchukua nafasi hiyo.


1. SEAN DYCHE;

Kocha huyo mwenye uzoefu kwa sasa hana kazi baada ya kufukuzwa Nottingham Forest mwezi uliopita. Dyche mwenye miaka 54 alisema hakuelewa uamuzi huo, akisema timu yake ilikuwa nafasi ya tisa kwenye msimamo wa Ligi Kuu England wakati akiwa kocha. Kocha huyo wa zamani wa Everton na Burnley anaweza kufurahia nafasi ya kuisaidia Spurs kubaki Ligi Kuu.


2. RYAN MASON

Mason tayari amewahi kuwa kocha wa muda wa Tottenham mara mbili. Mchezaji huyo wa zamani wa Spurs mwenye miaka 34 amekuwa sehemu ya klabu hiyo kwa takribani miaka 27 kama mchezaji wa akademi, mchezaji wa kikosi cha kwanza, kocha wa vijana, kocha wa muda na msaidizi. Aliondoka kwenda kufundisha West Bromwich Albion msimu uliopita lakini alifukuzwa Januari. Faida yake ni kwamba anaheshimika na wachezaji wengi wa Spurs.


3. ROBERTO DE ZERBI

Badala ya kuleta kocha wa muda, Spurs inaweza kuamua kumteua moja kwa moja kocha wa kudumu. Kocha huyo wa zamani wa Brighton anapendwa kwa mtindo wake wa soka la kushambulia. Hata hivyo, bado haijulikani kama Mtaliano huyo angefaa katika vita ya kujiokoa kushuka daraja.

4. ROBBIE KEANE

 Nyota huyo wa zamani wa Tottenham ameanza kazi yake ya ukocha kwa namna ya kipekee. Baada ya kufanya kazi kama kocha msaidizi, alichukua nafasi ya ukocha wa Maccabi Tel Aviv na kushinda ligi na kombe nchini Israel. Kwa sasa anafundisha Ferencvárosi TC nchini Hungary. Keane amesema hataki kurudi Spurs kama kocha wa muda, hivyo klabu italazimika kuamua kama anaweza kuwa kocha wa muda mrefu.


5. MAURICIO POCHETTINO

Kocha huyo wa Argentina amekuwa akihusishwa sana na kurejea Tottenham. Alikuwepo uwanjani wakati wa mechi dhidi ya Atlético Madrid. Kwa sasa ni kocha wa timu ya taifa ya Marekani na swali kubwa ni kama anaweza kuunganisha kazi hiyo na kurejea Spurs kabla ya msimu ujao.


6. HARRY REDKNAPP

 Redknapp ni kocha anayependwa sana Tottenham baada ya kufanya kazi nzuri katika klabu hiyo kati ya 2008 na 2012. Kocha huyo mwenye miaka 79 alisema angekubali kazi hiyo kama angepewa nafasi. Hajafundisha timu tangu alipokuwa kocha wa Birmingham City mwaka 2017, lakini ana uzoefu mkubwa wa kushughulika na wachezaji.


7.RUBEN AMORIM

 Jina lingine linalotajwa ni kocha wa zamani wa Manchester United. Mreno huyo mwenye miaka 41 alifukuzwa Januari baada ya kutofautiana na mkurugenzi wa michezo, Jason Wilcox. Alikuwa pia kwenye orodha ya Tottenham mwaka 2023 kabla klabu haijamchagua Ange Postecoglou. Hata hivyo, mashabiki wengi wanaweza kukata tamaa ikiwa Spurs itamchagua kocha aliyeshindwa katika fainali ya UEFA Europa League msimu uliopita.