Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Makinda wa kutazamwa Ligi Mabingwa Ulaya msimu huu

LONDON, ENGLAND . LIGI Mabingwa Ulaya imerudi kwa kishindo je wachezaji gani vijana ambao wanaweza kung’ara kwenye michuano hiyo msimu huu wa 2023-2024?

Hakuna mashindano yanayovumbua vipaji vipya kwenye ramani ya soka kama Ligi Mabingwa Ulaya. Mastaa wa soka, Julian Alvarez, Kylian Mbappe na Erling Haaland waliibuka kusikojulikana lakini sasa wametengeneza majina makubwa kwenye historia ya michuano hiyo kutokana na kuweka rekodi mbalimbali. Hawa hapa madogo janja wa kutazamwa zaidi kwenye michuano hiyo msimu huu wa 2023-2024.


Alejandro Garnacho (Man United)

Kinda huyo alitimiza umri wa miaka 19 hivi karibuni, lakini winga huyo tayari ametengeneza jina lake tangu alipopandishwa kikosi cha kwanza. Kutokana na kutokuwapo Antony na Jadon Sancho kikosini, kocha Erik ten Hag huenda akampanga kwenye mechi za makundi msimu huu. Kinda huyo alikuwa na mchango mkubwa kila anapoingia akitokea benchini msimu uliopita.


Gavi (Barcelona)

Kinda huyo licha ya kuwa na umri wa miaka 18 tayari ameshacheza zaidi ya mechi 100, pia ameiwakilisha timu ya taifa ya Hispania kwenye jumla ya mechi 23, ukiongelea kuhusu kipaji cha kucheza soka hilo ni jambo lingine. Sasa ni kiongozi katika kikosi cha Xavi na amekuwa mchezaji muhimu kutokana na uwezo wake wa kutumia nguvu, ubunifu anapokuwa uwanjani. Amepewa nafasi kubwa kikosini na alifunga bao kwenye ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Antwerp kwenye mechi ya kwanza ya hatua ya makundi.


Arda Guler (Real Madrid)

Ingawa kinda huyo aliukosa mchezo wa kwanza wa Ligi Mabngwa Ulaya dhidi ya Union Berlin baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti, kuna matumaini kwamba kinda huyo atakuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi cha Carlo Ancelotti siku za usoni. Guler mwenye umri wa miaka 18 alisajiliwa kwa Pauni 17 milioni kipindi cha usajili wa kiangazi, ana wastani wa kuhusika na mabao na kutoa asisti kila baada ya dakika 91 tangu alipokiwasha Fenerbahce msimu wa 2021-22.


Rico Lewis (Man City)

Man City imeendelea kupata faida baada ya kuuza makinda wao hatari kama Cole Palmer ambaye alijiunga na Chelsea kwa Pauni 43 milioni. Lakini Pep Guardiola aligoma kumuachia kinda Rico Lewis kwani alikuwa hatari msimu uliopita. Beki huyo mwenye umri wa miaka 18 anaweza kupewa nafasi kwenye mechi za makundi kutokana Man City kuwa na kikosi kipana.


Youssoufa Moukoko (Borussia Dortmund)

Moukoko alicheza mechi yake ya pili ya Ligi Mabingwa Ulaya dhidi ya Paris Saint-Germain hata hivyo wakachezea kichapo cha mabao 2-0. Kinda huyo ana matumaini atakuwa fiti zaidi ili kuiwakilisha timu yake kwenye michuano hiyo mikubwa Ulaya. Dortmund ilipomsajili Niclas Fullkrug kwenye usajili wa dirisha la kiangazi ilitishia nafasi yake lakini Moukoko anaamini atamshawishi kocha Edin Terzic ampange kikosi cha kwanza kwenye michuano hii msimu huu.


Cher Ndour (PSG)

Uchezaji wake unafananishwa na Paul Pogba jinsi anavyokimbia kwa staili ya aina yake na jicho la kuona pasi. Kinda huyo alijiunga na Paris Saint-Germain akitokea Benfica kwenye dirisha la usajili la kiangazi anaweza kuwa mchezaji muhimu baada ya Neymar na Lionel Messi kuondoka endapo atapewa nafasi mara kwa mara.


Mathys Tel (Bayern Munich)

Baada ya ujio wa Harry Kane kikosini ilisemekana kinda huyo angetolewa kwa mkopo, akaongeze uzoefu sehemu nyingine hata hivyo akaamua kubaki Bayern. Kinda huyo aliyesajiliwa kwa Pauni 24.5 milioni kutoka Rennes, alifunga mabao mawili na kutoa asisti moja na kumshawishi Thomas Tuchel ambaye ameendelea kumuamini msimu huu. Ana wastani wa kuhusika na mabao kila dakika 80 tangu alipotua Allianz Arena mwaka jana.


Lamine Yamal (Barcelona)

Amekuwa gumzo baada ya kuiwakilisha timu ya taifa ya Hispania na Barcelona akiwa na umri wa miaka 16. Winga huyo tayari ameonyesha ubora wake na ametabiriwa kufanya makubwa tangu Lionel Messi alipofanya hivyo. Kinda huyo amekuwa mchezaji wa kwanza kinda kucheza mechi ya kwanza na kufunga bao kwa taifa lake. Vilevile alishafanya mambo ya kuvutia kwenye LaLiga alipopewa nafasi na kocha Xavi Hernandez.


Karim Konate (Red Bull Salzburg)

Straika huyo wa kimataifa wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 16 alifunga mabao sita katika mechi nane alizocheza msimu huu. Mashabiki wana hamu ya kumuona kwenye michuano hiyo mikubwa Ulaya baada ya kuaminia asilimia 100.


Warren Zaire-  Emery (PSG)

Kinda huyo aliweka rekodi ya kuwa mchezaji mdogo zaidi kuanza kwenye mechi za mtoano ya Ligi Mabingwa Ulaya msimu uliopita na ameendelea kuwa tegemeo PSG eneo la kati. Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 17 amekuwa mchezaji wa kikosi cha kwanza chini ya kocha Luis Enrique, kilichoshinda mechi ya kwanza ya makundi dhidi ya Borussia Dortmund kwa mabao 2-0. Moto mbona utawaka msimu huu. Tusubiri tuone.