Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Majeraha ya ajabu kwa wanasoka

MAJERAHA Pict

Muktasari:

  • England ilitinga hatua ya robo fainali baada ya kuibuka na ushindi wa kusisimua wa mabao 3-2 dhidi ya Mexico, moja ya mataifa mwenyeji wa mashindano hayo.

MIAMI, MAREKANI: BABA wa kiungo wa England, Jordan Henderson, amefichua kuwa mwanawe alivunjika vibaya mkono wa kushoto wakati wa kusherehekea ushindi dhidi ya Mexico katika Kombe la Dunia.

England ilitinga hatua ya robo fainali baada ya kuibuka na ushindi wa kusisimua wa mabao 3-2 dhidi ya Mexico, moja ya mataifa mwenyeji wa mashindano hayo.

Hata hivyo, furaha ya ushindi iligeuka majonzi baada ya Henderson, mwenye umri wa miaka 36, kuanguka vibaya alipokuwa akijaribu kuruka mabango ya matangazo yaliyokuwa pembeni mwa uwanja ili kusherehekea na mashabiki.

Beki Dan Burn, ambaye tayari alikuwa ameruka uzio huo, alitambua haraka uzito wa tukio hilo na kuwaashiria wahudumu wa afya kuingia uwanjani kwa dharura kumsaidia kiungo huyo.

Baada ya kufanyiwa vipimo, ilibainika kuwa Henderson alivunjika vibaya mfupa wa mkono wake wa kushoto, hali iliyomlazimu kuondolewa katika kikosi cha England kwa mechi zote zilizosalia za Kombe la Dunia.

Kiungo huyo, ambaye aliwahi kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England, sasa anatarajiwa kufanyiwa upasuaji ili kurekebisha jeraha hilo.

Baba yake, Brian Henderson, ameelezea kwa kina namna jeraha hilo lilivyokuwa baya, akisema mwanawe "aliuvunja kabisa mfupa wa mkono wa kushoto" wakati wa shangwe za ushindi, tukio ambalo limekatisha safari yake katika mashindano hayo.

Henderson si mchezaji wa kwanza kuumia kwa njia isiyo ya kawaida. Hapa chini ni baadhi ya majeraha ya kushangaza yaliyowahi kuwakumba nyota mbalimbali wa soka.

MAJE 01

Michael Stensgaard: Alijeruhiwa na meza ya kupigia pasi

Kipa wa zamani wa Liverpool, Michael Stensgaard, alitengua bega mwaka 1994 alipokuwa akikunja ubao wa kupigia pasi nyumbani.

Jeraha hilo liliongeza matatizo ya bega aliyokuwa nayo awali na hatimaye likamlazimu kustaafu soka akiwa na miaka 26 tu.

MAJE 02

Kevin-Prince Boateng: Maisha ya faragha chumbani.

Nyota wa zamani wa Tottenham Hotspur, Kevin-Prince Boateng, aliwahi kudaiwa kuumia mara kwa mara kutokana na maisha yake ya kimapenzi.

Mwaka 2012, aliyekuwa mke wake, Melissa Satta, amesema majeraha ya Boateng yalichangiwa na kufanya mapenzi mara nyingi kila wiki.

MAJE 03

Richard Wright: Alianguka kutoka kwenye dari

Golikipa wa zamani wa Everton, Richard Wright, aliumia bega mwaka 2003 baada ya kuanguka kutoka kwenye sehemu ya juu ya nyumba (attic).

Baadaye, mwaka 2006, pia alijiumiza kifundo cha mguu baada ya kukanyaga bango lililoandikwa "Usifanyie mazoezi hapa" kabla ya mechi dhidi ya Chelsea.

MAJE 04

Lee Beevers: Alikwazwa na kigari cha mtoto

Beki wa zamani Lee Beevers aliteguka vibaya alipokuwa akibeba kigari cha mtoto wake ngazini, hali iliyosababisha mfupa wa mkononi kuteguka.

MAJE 05

Wojciech Szczesny: Ajali ya kunyanyua vyuma

Golikipa Wojciech Szczesny alivunja mikono yote miwili akiwa na miaka 17 baada ya kuteleza wakati wa mazoezi ya kunyanyua vyuma.

Hata hivyo, baadaye alifanikiwa kuwa golikipa namba moja wa Arsenal, kabla ya kuchezea Juventus na Barcelona.

MAJE 06

Frenkie de Jong: Alidungwa na nyuki

Mwaka 2020, kiungo wa FC Barcelona, Frenkie de Jong, alipata uvimbe mkubwa mkononi baada ya kudungwa na nyuki.

MAJE 07

Dave Beasant: Chupa ya salad cream

Kipa wa zamani Dave Beasant alivunja kidole cha mguu baada ya kujaribu kuizuia kwa mguu chupa ya salad cream iliyokuwa ikianguka.

Jeraha hilo lilimweka nje ya uwanja kwa miezi miwili.

MAJE 08

Alan Wright: Ferrari yake ilimsababishia jeraha

Beki wa zamani wa Aston Villa, Alan Wright, aliumia goti alipokuwa akijaribu kufikia pedali za gari lake la Ferrari.

MAJE 09

Kirk Broadfoot: Mayai yaliyolipuka

Beki wa zamani wa Rangers, Kirk Broadfoot, aliungua usoni baada ya yai alilokuwa akipika kwenye microwave kulipuka alipoinama kulitazama.

Marco Asensio: Chunusi baada ya kunyoa vinyweleo vya miguu

Mwaka 2017, Marco Asensio alikosa mechi ya Ligi ya Mabingwa UEFA kutokana na chunusi iliyoota kwenye mguu baada ya kunyoa nywele za miguu.

Kocha Zinedine Zidane amesema hata kuvaa soksi kulimsababishia maumivu.

MAJE 10

Leroy Lita: Alijeruhiwa kwa kujinyoosha kitandani

Mshambuliaji wa zamani wa Reading, Leroy Lita, aliumia misuli ya mguu mwaka 2007 baada ya kujinyoosha kitandani alipokuwa anaamka.

MAJE 11

David Batty: Aligongwa na baiskeli ya mtoto

Kiungo wa zamani wa Leeds United, David Batty alicheleweshwa kupona baada ya kugongwa na baiskeli ya magurudumu matatu aliyokuwa akiendesha binti yake wa miaka miwili.

MAJE 12

Rio Ferdinand: Michezo ya video

Beki wa zamani wa Manchester United, Rio Ferdinand, alijiumiza kano nyuma ya goti baada ya kukaa kwa muda mrefu akicheza mchezo wa video wa Pro Evolution Soccer huku miguu yake ikiwa juu ya meza.

MAJE 12 (1)

Rami Kaib: Karoti mbichi

Mwaka 2021, beki Rami Kaib alivunja taya alipokuwa akila karoti mbichi, baada ya tayari kuwa amepata pigo kwenye mechi iliyotangulia.

MAJE 14

Victor Adeboyejo: Chafya kali

Mshambuliaji wa zamani wa Bolton Wanderers, Victor Adeboyejo, alikosa mchezo mwaka 2024 baada ya chafya kali kusababisha maumivu makali kwenye mbavu.

MAJE 15

Axel Tuanzebe: Alijeruhiwa akiosha vyombo

Beki wa zamani wa Manchester United, Axel Tuanzebe, alipasua vibaya kidole gumba baada ya glasi kuvunjika alipokuwa akiosha vyombo mwaka 2024.

Madaktari waliogopa huenda angepoteza kidole hicho, lakini upasuaji ulifanikiwa kukiokoa.

MAJE 16

David James: Rimoti ya televisheni

Kipa wa zamani wa England, David James, aliwahi kuumia mgongo alipokuwa akijinyoosha kuifuata rimoti ya televisheni.

Katika tukio jingine, aliumia bega alipokuwa akivua samaki.