Maguire akubali lawama zote

MANCHESTER, ENGLAND. BEKI na kapteni wa zamani wa Manchester United Harry Maguire amesema huwa anajisikia furaha pale anapoonyeshewa vidole na kusemwa kwa sababu jambo hilo huwaondoshea presha wachezaji wenzake na kuwafanya wacheze vizuri.

Maguire ambaye amejumuishwa kwenye kikosi cha msimu cha Man United, hivi karibuni amekuwa akitajwa sana mitandaoni na kwenye vyombo mbali mbali vya habari Dunia baada ya kujifunga kwenye mchezo kati ya England na Scotland kwenye mchezo wa kirafiki ambao ulimalizika kwa England kushinda mabao 3-1.

'Ni jambo zuri kwangu kwa sababu huwapunguzia presha wachezaji wenzangu kwa sababu kila mtu huwa ananisema na kunitazama mimi, hiyo huwafanya wenzangu wacheze vizuri"

“Mimi sio mchezaji ambaye nina upungufu wa afya ya akili, nimekuwa nikipitia hii hali ya kussema kwa muda mrefu sasa ukizingatia nimekuwa mchezaji na kapteni wa Man United ka karibia  miaka minne, ingawa siwezi kusema napenda ama nimezoea moja kwa moja"

“Nilipokuwa kapteni wa Man United ilikuwa  ni heshima kwangu kwa kupewa majukumu mengi ambayo yaliambatana na mambo mbali mbali na muda mwingine nilikuwa nikijisikia vibaya"

Kocha wa England Gareth Southgate ameonyesha kuchukizwa na watu wanaomsema vibaya beki huyo ambaye amekuwa na wakati mgumu kwenye kikosi cha Man United kwa muda mrefu.

Tangu kuanza kwa msimu huu Maguire amecheza mechi moja tu ambayo ilikuwa ni dhidi ya Arsenal akiingia akitokea benchi.

Baada ya msimu huu kuanza pia alinyang'anywa kitambaa cha unahodha ambacho amekabidhiwa Bruno Fernandes na alikuwa akihusishwa kuwa kwenye mchakato wa kutaka kutimkia West Ham lakini dili lilifeli katika dakika za mwisho baada ya kushindwa kufikia muafaka.

Alipoulizwa kwanini dili hilo lilifeli Magu mwenye umri wa miaka, 30,  alisema kuwa walishindwa kufikia muafaka baada ya mazungumzo ya muda.

“Sikufikia mwisho wa makubaliano, Man United ilikuwa na furaha yamimi kusalia kwenye timu na mimi nina furaha ya kusalia hapa na kuendelea kupambania nafasi kwenye kikosi cha kwanza"

"Nitapambana kwenye mazoezi na kutoa kila kitu kuhakikisha napata nafasi, bado nahitaji kucheza mpira,"

Beki huyu ambaye alisajiliwa akitokea Leicester City kwa ada ya uhamisho ya Euro...milioni mwaka amefunguka kuwa moja ya sababu zilizosababisha asipate nafasi ya kucheza kwenye mechi kadhaa za mwanzoni mwa msimu ilikuwa ni uchache wa michezo hiyo.

"Wiki nne za kwanza zilikuwa ngumu kwa sababu kulikuwa na mechi moja tu ndani ya wiki na kocha hakunichagua, lakini wiki zijazo kutakuwa na mechi nyingi na nina uhakika nitacheza mechi nyingi.