Madueke pigo lingine Arsenal
Muktasari:
- Madueke (23), alilazimika kuondoka uwanjani wakati wa mapumziko katika mechi Jumapili baada ya kuumia na kocha Mikel Arteta alisema kuwa hakuwa vizuri.
LONDON, ENGLAND: WINGA wa Arsenal, Noni Madueke anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa takriban miezi miwili kutokana na jeraha la goti alilopata dhidi ya Manchester City.
Madueke (23), alilazimika kuondoka uwanjani wakati wa mapumziko katika mechi Jumapili baada ya kuumia na kocha Mikel Arteta alisema kuwa hakuwa vizuri.
Mchezaji huyo ambaye alijiunga na Arsenal dirisha lililopita la majira ya kiangazi, alifanyiwa vipimo zaidi Jumatatu na tovuti ya Athletic imefichua kuwa ripoti ya daktari inaonyesha atakuwa nje kwa miezi miwili na anaweza kurejea katikati ya Novemba.
Madueke anaweza kurejea na kucheza dhidi ya Chelsea pamoja na Tottenham ambazo zote zinapigwa mwishoni mwa Novemba.
Kiungo huyo alilazimika kuondoka uwanjani wakati wa mapumziko katika mchezo huo uliomalizika kwa sare ya bao 1-1 na nafasi yake ikachukuliwa na Bukayo Saka ambaye naye alikuwa akirejea baada ya jeraha la misuli ya nyuma ya mguu lililomweka nje kwa zaidi ya wiki mbili.
Wakati anatoka awali ilidhaniwa kuwa yalikuwa ni mabadiliko ya kiufundi, lakini Mikel Arteta alisema baada ya mechi kuwa alikuwa na shida ambayo baadae ilibainika kuwa ni jeraha la goti la kulia.
Baada ya mechi Arteta alisema: “Alipata shinda mapema na hakuwa tayari kuendelea.” Madueke alijiunga na Arsenal kutoka Chelsea kwa uhamisho la Pauni i 52 msimu ameonyesha kiwango bora na kuwaziba midomo baadhi ya waliokuwa wanakosoa usajili wake. Madueke pia ameonyesha kiwango akiwa na timu ya taifa ya England katika mapumziko ya hivi karibuni ya kimataifa.
Thomas Tuchel alimwingiza katika mechi za kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Andorra na Serbia, na nyota huyo alifunga bao katika ushindi wa 5-0 dhidi ya Serbia.
Arsenal imekuwa na shida ya majeraha msimu huu na hadi sasa inamkosa nahodha Martin Odegaard anayesumbuliwa na tatizo la bega kwa muda mrefu, Kai Havertz alifanyiwa upasuaji wa goti mwezi uliopita, pia Gabriel Jesus ameendelea kuuguza majeraha.