Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Madrid yapanga kuitibulia Liverpool kwa Guehi

Muktasari:

  • Guehi alishafanya hadi vipimo vya afya kabla ya dili kufeli katika dakika za mwisho katika dirisha lililopita baada ya kocha wa Palace, Oliver Glasner kutishia kwamba ikiwa staa huyo atauzwa bila ya kupatikana kwa mbadala wake basi yeye angejiuzulu kuifundisha timu hiyo.

REAL Madrid inapiga hesabu za muda mrefu kuingia katika vita dhidi ya Liverpool mwakani ili kuipata saini ya beki kisiki wa Crystal Palace na timu ya taifa ya England, Marc Guehi.

Guehi alishafanya hadi vipimo vya afya kabla ya dili kufeli katika dakika za mwisho katika dirisha lililopita baada ya kocha wa Palace, Oliver Glasner kutishia kwamba ikiwa staa huyo atauzwa bila ya kupatikana kwa mbadala wake basi yeye angejiuzulu kuifundisha timu hiyo.

Ripoti zinaeleza Liverpool imemweka kiporo staa huyo hadi mwakani ambapo inaweza kuwasilisha ofa ya kutaka kumsajili aidha katika dirisha la majira ya baridi ambapo itampata kwa pesa kiduchu au mwisho wa msimu ambapo mkataba wake utakuwa unamalizika.

Hata hivyo, mpango wao huo huenda ukawa mgumu kutimia kwa sababu Madrid pia imeanza kuinyemelea saini yake jambo litakalozidisha ushindani zaidi itakapofika muda wa usajili.

Liverpool inamwinda kwa sababu inamwona kama mbadala sahihi wa Virgil van Dijk ambaye umri ushaanza kumtupa mkono.


Danny Welbeck

  MANCHESTER United ilikuwa na mpango wa kumunua  Danny Welbeck kutoka Brighton katika dirisha lililopita la majira ya  kiangazi.

 Hata hivyo, mmiliki mwenza Sir Jim Ratcliffe hakukubali mchakato huo kuendelea.Welbeck, 35, aliwahi kuichezea Man United hapo awali kabla ya kuuzwa kwenda Arsenal mwaka 2014.

Mkataba wake wa sasa ambao unamwezesha kukunja Pauni 70,000 kwa wiki unafikia tamati mwisho wa msimu huu.


Andre Onana

MABOSI wa Manchester United wapo tayari kumuuza kipa wao wa kimataifa wa Cameroon, Andre Onana, 29, ndani ya siku chache zijazo kwenda Uturuki au Saudi Arabia wakiwa na lengo la  kupunguza gharama za mishahara.

Onana alijiunga na Man United mwaka 2023 akitokea Inter Milan kwa dau la Pauni 47 milioni, lakini hivi karibuni amekuwa akikosolewa kwa makosa ya mara kwa mara.


Yves Bissouma

TOTTENHAM  Hotspur bado ina mpango wa  kumuuza kiungo wake wa kimataifa wa Mali, Yves Bissouma, 29, ambaye haonekani kuwa tegemeo kwa kocha Thomas Frank.

Timu kadhaa kutoka Saudi Arabia na Uturuki ambako madirisha ya usajili bado yako wazi zimekuwa zikihusishwa naye.

Bissouma alisajiliwa Spurs mwaka 2022 akitokea Brighton kwa takriani Pauni 25 milioni.


Patrick Bamford

MABINGWA wa Scotland, Celtic wapo katika mazungumzo na wawakilishi wa mshambuliaji wa zamani wa Leeds United, Patrick Bamford, 31, ambaye amemaliza mkataba wake na Leeds United ulimalizika mwisho wa mwezi uliopita.

Ikiwa makubaliano yatafikiwa, Bamford atatua Celtic muda wowote kwani licha ya dirisha la usajili kufungwa, mchezaji ambaye yupo huru anaruhusiwa kusajiliwa.


Senne Lammens

ASTON Villa inadaiwa kuwa ilishafanya makubaliano na Royal Antwerp kwa ajili ya kumsajili kipa wa timu hiyo, Senne Lammens lakini mambo yaliharibika baada ya mchezaji mwenyewe kugoma na kusisitiza kwamba anataka kwenda Man United. Villa ilikuwa imeweka mezani ofa ya Pauni 18.1 milioni kama ada ya uhamisho ambayo Antwerp iliikubali.


Emiliano Martinez

KIPA wa Aston Villa, Emiliano Martinez amekataa ofa kutoka Galatasaray ya Uturuki ambayo ilikuwa tayari kumsajili baada ya dili lake la kujiunga na Manchester United kufeli katika siku ya mwisho ya dirisha la usajili. Martinez, 33, ameiambia Galatasaray kwamba timu pekee aliyohitaji kujiunga nayo katika dirisha hili ni Man United pekee. Mkataba wake unaisha mwaka 2028.


Yoane Wissa

MSHAMBULIAJI wa Newcastle na timu ya taifa ya DR Congo, Yoane Wissa, 29, alikamilisha uhamisho wake wa dakika za mwisho kutoka Brentford kwenda Newcastle United ikiwa zimebakia sekunde 30 pekee kabla ya dirisha kufungwa. Dili hilo lilikuwa karibu kuharibika kwa sababu Wissa alisahau kusaini moja ya fomu muhimu. Wissa amejiunga na Newcastkekuchukua nafasi ya Alexander Isak, ambaye ametimkia Liverpool.