Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mac Allister aikataa Madrid, kuna jambo linaendelea

Muktasari:

  • Inaelezwa Mac Allister kwa sasa ana furaha kuendelea kuitumikia Liverpool na hafikirii kabisa kuiacha klabu hiyo.

KIUNGO wa Liverpool na timu ya taifa ya Argentina, Alexis Mac Allister, 27, ana mpango wa kufanya mazungumzo na majogoo  kuhusu mkataba mpya ifikapo mwisho wa msimu huu  licha ya kuhusishwa na Real Madrid.

Inaelezwa Mac Allister kwa sasa ana furaha kuendelea kuitumikia Liverpool na hafikirii kabisa kuiacha klabu hiyo.

Kwa sasa ana mkataba unaotarajiwa kumalizika mwaka 2028 na msimu huu amecheza mechi 41 za michuano yote, amefunga mabao matano na kutoa asisti nne.

Mabosi wa Liverpool walikuwa tayari kuchukua pesa na kumuuza ikiwa  Mac Allister mwenyewe angekuwa tayari kuondoka mwisho wa msimu.

Licha ya mchezaji mwenyewe kutoonyesha nia ya kutaka kutua Madrid ripoti zinadai Madrid bado haijachoka na itaendelea kumshawishi kwani inahitaji sana kiungo dirisha la majira ya kiangazi ili kuboresha kikosi chao ambacho licha ya kuwa na nafasi bora ya ushambuliaji inakosa mtu wa kuilisha inavyotakiwa.


Djed Spence

MIAMBA ya Italia, Juventus, imeonyesha nia ya kumsajili beki wa kulia wa Tottenham Hotspur na timu ya taifa ya England, Djed Spence, 25, dirisha lijalo  la usajili la majira ya kiangazi. Inaelezwa Juventus inataka kuongeza nguvu katika safu yake ya ulinzi na Spence ameonekana kuwa mmoja wa wachezaji wanaoweza kuleta ushindani mkubwa upande wa kulia. Spence amekuwa akipata nafasi kubwa ya kucheza Tottenham. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2029.


Moussa Diaby

LIVERPOOL inafikiria kwa uzito uwezekano wa kumsajili winga wa kimataifa wa Ufaransa, Moussa Diaby, 26, kutoka Al-Ittihad Club ya Saudi Arabia dirisha la usajili la majira ya kiangazi. Inaelezwa Diaby, ambaye zamani aliwahi kuitumikia Aston Villa, amewekwa katika rada na Liverpool kwa sababu inaamini kwa asilimia kadhaa anaweza akaziba pengo la Mohamed Salah ambaye huenda akaondoka mwisho wa msimu. Diaby mwenyewe anaonekana kuwa tayari kurudi England ingawa inaeleweka majogoo hao hawatoweza kumpa pesa sawa na ile ambayo anaipata kwa sasa.


Bruno Guimaraes

TAARIFA za ndani zinadai mabosi wa Newcastle United F.C. hawana  mpango wa kumuuza kiungo wake nyota wa kimataifa wa Brazil, Bruno Guimaraes, 28, licha ya kuvutiwa naye na Manchester United F.C. Inaelezwa Newcastle tayari imeanza mazungumzo ya kumpa mkataba mpya kiungo huyo ili kumshawishi aendelee kubaki katika kikosi hicho kwa muda mrefu zaidi. Guimaraes amekuwa mmoja wa wachezaji muhimu ndani ya Newcastle tangu alipojiunga na klabu hiyo. Kwa sasa ana mkataba unotarajiwa kumalizika mwaka 2028. Vigogo wa Newcastle wanaamini kuwa kumbakisha kiungo huyo ni sehemu muhimu ya mpango wao wa kuendelea kujenga kikosi imara.


Tino Livramento

BEKI wa Newcastle United, Tino Livramento, 23, bado hayuko karibu kufikia makubaliano binafsi na Manchester City ambayo inahitaji kumsajili dirisha la majira ya kiangazi. Kwa sasa kumekuwa na uvumi mwingi unaomhusisha Livramento na kuhamia Manchester City, lakini hadi sasa hakuna mazungumzo ya karibu yaliyofanyika kati ya Newcastle na matajiri hao wa Jiji la Manchester. Beki huyo amekuwa akionyesha kiwango kizuri tangu alipojiunga na Newcastle mwaka 2028.


Scott McTominay

NAPOLI inataka kumwongeza muda wa mkataba wa kiungo wao wa kimataifa wa Scotland, Scott McTominay, 29, hadi kufikia  mwaka 2030. Ripoti zinaeleza Napoli imeanza mipango ya kumuongezea mkataba staa huyo ili kuzuia uwezekano wa klabu nyingine kujaribu kumsajili dirisha la usajili la majira ya kiangazi.

McTominay amekuwa mmoja wa wachezaji muhimu katika safu ya kiungo ya Napoli kutokana na uwezo wake wa kukaba na kufunga.

Hivi karibuni timu kadhaa kutoka England ikiwemo klabu yake ya zamani, Manchester United


Callum Wilson

MSHAMBULIAJI wa West Ham United F.C, Callum Wilson, 34, amefikia makubaliano ya kimazungumzo kusaini mkataba mpya wa mwaka mmoja na klabu hiyo. Inaelezwa Wilson alikuwa akihitaji kutimkia Celtic F.C. ya Scottland lakini amebadilisha maamuzi na ameamua kubaki West Ham walau msimu mmoja zaidi. Uzoefu wa mshambuliaji huyo unaonekana kuwa sababu kubwa ya klabu hiyo ya London kutaka kuendelea kuwa naye ndani ya kikosi chao.


Cavan Sullivan

MANCHESTER City imeonyesha haitamchukua kiungo chipukizi wa Marekani, Cavan Sullivan, 16, kujiunga nao msimu ujao kutoka Philadelphia Union ambako wamemtoa kwa mkopo baada ya kumnunua. Ripoti zinaeleza Manchester City kwa sasa haiamini kama ni wakati sahihi kumchukua kiungo huyo na wanahitaji aendelee kukua zaidi. Inaelezwa vigogo hao wanataka Sullivan acheze kwa msimu mmoja zaidi kabla ya kumchukua rasmi kwa ajili ya kuwatumikia.