Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Liverpool yatoa ofa ya mwisho

LIVER Pict

Muktasari:

  • Guehi ambaye ni kapteni wa Palace amekuwa akiwindwa na Liverpool kwa muda mrefu kutokana na kiwango bora alichoonyesha akiwa na klabu na timu ya taifa.

LONDON, ENGLAND: LIVERPOOL imeweka mezani ofa ya mwisho ya pauni 40 milioni kwenda Crystal Palace ili kumsajili beki Marc Guehi katika dirisha hili na ripoti zinaeleza haitatoa tena ofa nyingine endapo hiyo itakataliwa.

Ripoti zinaeleza ofa hiyo ina nafasi kubwa ya kufanikisha usajili wa beki huyo wa kati, ambaye ametimiza miaka 25 jana.

Guehi ambaye ni kapteni wa Palace amekuwa akiwindwa na Liverpool kwa muda mrefu kutokana na kiwango bora alichoonyesha akiwa na klabu na timu ya taifa.

Beki huyu kisiki aliyeshinda Kombe la FA msimu uliopita, yuko katika mwaka wa mwisho wa mkataba wake, na yuko tayari kujiunga la Liverpool licha ya kuwa pia anawindwa na Arsenal, Chelsea na Newcastle.

Guehi alicheza dakika 45 katika mechi ya kirafiki  dhidi ya Millwall juzi, na inaelezwa hana mpango wa kulazimisha kuondoka na timu yake itakapoona dau litakalowasilishwa ni sahihi atakuwa tayari kuondoka,

Kwa mujibu wa vyanzo vya ndani, Guehi ni mmoja wa wachezaji ambao hawajali sana kuhusu pesa bali wanaangalia zaidi soka.

Licha ya kubakisha mwaka mmoja katika mkataba wake ambao alisaini mwaka 2021 alipojiunga nao akitokea Chelsea, Guehi amekuwa akikataa ofa za kuongeza mkataba mpya alizowekewa mezani na Palace.

Palace haitaki ofa za mabadilishano ya wachezaji, ingawa Liverpool wako tayari kutoa wachezaji kama Ben Doak mwenye umri wa miaka 19 pamoja na kiasi cha pesa.

Timu hiyo yenye maskani yake Jijini London inahitaji pesa taslimu ili kusajili mchezaji mpya atakayeziba pengo la Guehi.

Kocha wao Oliver Glasner wamewaambia mabosi Palace kuwa anahitaji mabeki wapya wawili kwa ajili ya msimu ujao na kutokana na jambo hilo, timu hiyo inatazamia zaidi kuuza kwa pesa ndefu ili iweze kuzitumia katika sajili hizo.

Chaguo la kwanza la kocha Glasner endapo Guehi atauzwa ni beki wa Sporting Lisbon, Ousmane Diomande  mwenye umri wa miaka 21, lakini ikishindikana anataka asajiliwe hata Tiago Djalo, 25, wa Juventus na timu ya taifa ya Ureno.