Liverpool yaipiga Man United, Chelsea yachapwa

Muktasari:
- Huu ulikuwa mchezo wa mwisho kwa timu zote, huku Manchester United ikitarajiwa kuvaana na Manchester City kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii Jumamosi ijayo katika Uwanja wa Wembley.
LIVERPOOL, ENGLAND: Liverpool imemaliza kwa mkwara mzito maandalizi ya msimu mpya wa 2024/2025 baada ya kuichapa Manchester United mabao 3-0 kwenye mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Williams Brice nchini Marekani.
Huu ulikuwa mchezo wa mwisho kwa timu zote, huku Manchester United ikitarajiwa kuvaana na Manchester City kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii Jumamosi ijayo katika Uwanja wa Wembley.
Liverpool ikiwa chini ya kocha mpya Arne Slots, imefanikiwa kujipatia mabao yake kupitia kwa Fabio Carvalho dakika ya 10, Curtis Jones dakika ya 36 na Konstantinos Tsimkas dakika ya 61 ya mchezo.
Mechi nyingine kali ya kirafiki iliyopigwa alifajiri ya leo, Manchester City imemaliza mechi zake za maandalizi ya msimu kibabe baada ya kuichapa Chelsea mabao 4-2.
Earling Haaland amefunga mabao matatu dakika ya nne, tano na 56 na la nne likitupiwa na Oscar Bobb dakika ya 55, huku Chelsea ikifunga kupitia kwa Raheem Sterling dakika ya 59 na Nuno Madueka 89 ya mchezo huo wa mwisho kabla Man City haijavaana na Man United Jumamosi ijayo.