Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Liverpool wapewe ubingwa wao EPL

WAPEWE Pict

Muktasari:

  • Bao la Diogo Jota lilitosha kwa Liverpool kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya mahasimu wao hao na hivyo kujiweka kwenye nafasi nzuri kabisa ya kunyakua taji la Ligi Kuu England msimu huu. 

LIVERPOOL, ENGLAND: LIVERPOOL imerejea kwenye makali yake ya ushindi baada ya kuichapa Everton kwenye kipute cha Merseyside derby kilichofanyika Anfield, Jumatano iliyopita.

Bao la Diogo Jota lilitosha kwa Liverpool kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya mahasimu wao hao na hivyo kujiweka kwenye nafasi nzuri kabisa ya kunyakua taji la Ligi Kuu England msimu huu. 

Kikosi hicho cha Kocha Arne Slot bado kinaongoza msimamo wa ligi kwa tofauti ya pointi 12 na bado mechi nane tu msimu kufika mwisho. Vita ya kusaka ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu imebaki kwa timu mbili, Liverpool na Arsenal, lakini kwa hali ilivyo kwa sasa miamba ya Anfield inaelekea kushinda vita hiyo. Na swali lililobaki, lini watatangaza ubingwa?

Kutokana na hilo, zimeangaziwa mechi zao tano zijazo kwa kila timu kuona kama bingwa anaweza kupatikana.

Aprili 5: Everton vs Arsenal, Aprili 6: Fulham vs Liverpool

Wikiendi hii, Arsenal itakwenda kuikabili Everton huko Merseyside, wakati Liverpool itasafiri kwenda London kukipiga na Fulham. Majeraha yanatajwa kuwa tatizo kwenye kikosi cha Arsenal, lakini kurejea kwa Bukayo Saka uwanjani kumpa Kocha Mikel Arteta uhakika wa kushinda mechi. Liverpool inakwenda Fulham, ikitambua ugumu wa wapinzani wao hao, baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 kwenye mechi ya kwanza iliyofanyika Anfield mwanzoni mwa msimu huu.

Utabiri: Everton 1 Arsenal 2, Fulham 1 Liverpool 2 Pointi: Liverpool 76, Arsenal 64


Aprili 13: Liverpool vs West Ham

Arsenal imepata nafasi nyingine ya kutangulia kucheza na safari hii itakuwa Emirates kukipiga na Brentford, ambayo itakwenda uwanjani hapo baada ya mechi ya Real Madrid. Brentford ina washambuliaji tishio na hilo linafanya kuwapo kwa mtihani mzito kwa safu ya mabeki ya Arsenal, ambayo ina majeruhi wengi. 

Liverpool itasubiri kwa siku moja kabla ya kukkaribisha West Ham uwanjani Anfield, mechi ambayo unaziona kabisa pointi tatu kwa vijana wa Slot.

Utabiri: Arsenal 1 Brentford 1, Liverpool 2 West Ham 0

Pointi: Liverpool 79, Arsenal 65


Aprili 20: Ipswich vs Arsenal, Leicester vs Liverpool

Ni saa chache tu zinatofautisha mechi hizi, lakini Arsenal kwa mara nyingine inatangulia kucheza. 

Hiyo ni mechi nyingine ngumu kwao, kuwakabili Ipswich Town kwao, wakati Liverpool watasafiri hadi King Power kukipiga na Leicester City, mechi ambayo kwenye katarasi inayonekana kuwa nyepasi kwao.

Utabiri: Ipswich 1 Arsenal 3, Leicester 0 Liverpool 3

Pointi: Liverpool 82, Arsenal 68


Aprili 26: Arsenal vs Crystal Palace (imeahirishwa), Aprili 27: Liverpool vs Tottenham

Arsenal ilipangwa kutangulia kucheza, lakini wapinzani wao baada ya kutinga nusu fainali ya Kombe la FA, mechi hiyo imeahirishwa. Jambo hilo litaifanya Liverpool kuwa na nafasi ya kuongeza pengo la pointi, wakati itakapokuwa uwanjani Anfield kukabiliana na Tottenham Hotspur, ambayo imekuwa na mwendo wa kusuasua sana msimu huu. 

Liverpool itahitaji pointi tatu kwenye mechi hiyo, ambazo zinaweza kuwafanya kuwa mabingwa wa ligi msimu huu.

Utabiri: Liverpool 3 Tottenham 1

Pointi: Liverpool 85, Arsenal 68.


Mei 3: Arsenal vs Bournemouth, Mei 4: Chelsea vs Liverpool

Ikitokea Liverpool imeshindwa kutangaza ubingwa kwenye wiki iliyotangulia, itakuwa na nafasi ya kufanya hivyo uwanjani Stamford Bridge itakapokwenda kukipiga na Chelsea. 

Liverpool yenyewe inahitaji pointi 85 tu kuwa mabingwa wapya wa msimu huu. Kwenye wikiendi hii, Arsenal imetangulia pia kucheza, itakapokipiga na Bournemouth, siku moja kabla ya Liverpool kumalizana na Chelsea. 

Spurs ikigoma kufanywa ngazi na Liverpool, basi Stamford Bridge panaweza kugeuzwa ngazi na vijana hao wa Slot na kubeba ubingwa.

Utabiri: Arsenal 2 Bournemouth 1, Chelsea 2 Liverpool 2

Pointi: Liverpool 86 (mabingwa), Arsenal mwisho wao pointi 85.