Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Liverpool kupiga kibuti mastaa kibao

Muktasari:

  • Miamba hiyo ya Anfield inapewa nafasi kubwa ya kushinda ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu, lakini mwisho wa msimu inaweza kuachana na mastaa wake kibao dirisha la usajili litakapofunguliwa.

LIVERPOOL, ENGLAND: LIVERPOOL inakabiliwa na mchakato wa kuachana na mastaa wake kibao mwishoni mwa msimu huu bila ya kujali ni kitu gani kitatokea kwenye wiki hizi chache zilizobaki kabla ya msimu kumalizika.

Miamba hiyo ya Anfield inapewa nafasi kubwa ya kushinda ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu, lakini mwisho wa msimu inaweza kuachana na mastaa wake kibao dirisha la usajili litakapofunguliwa.

Masupastaa watatu, Mohamed Salah, Trent Alexander-Arnold na Virgil Van Dijk, wote mikataba yao itafika tamati mwishoni mwa msimu huu na hakuna makubaliano yaliyofikiwa juu ya kuongeza mikataba mipya kwenye kikosi hicho cha kocha Arne Slot.

Wakati ukiwaza itakuwaje Liverpool itakapoachana na miamba hiyo ya Anfield, lakini kuna uwezekano mkubwa wa kuwapo kwa wachezaji wengine wengi ambao wataonyeshwa mlango wa kutokea.

Kocha Slot na mabosi wake wa huko Anfield wanafahamu wazi kuna timu kibao za Ulaya zinahitaji wachezaji wao wa kikosi cha kwanza, beki Ibrahima Konate na mshambuliaji Luis Diaz.

Lakini, orodha haishii hapo tu kuna mastaa wengine kibao ambao huenda wakaachana na Liverpool wakati wa dirisha lijalo la majira ya kiangazi litakapofunguliwa ni pamoja na kipa Caoimhin Kelleher, Harvey Elliott, Joe Gomez, Darwin Nunez, Diogo Jota, Wataru Endo na Federico Chiesa.

Lakini pigo kubwa kwa mashabiki itakuwa kwa Salah, Van Dijk na Trent.

Licha ya Liverpool kutupwa nje kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya na kuchapwa kwenye fainali ya Kombe la Ligi, msimu wa kwanza wa kocha huyo Mdachi, Slot utahesabika kama wenye mafanikio kama atafanikiwa kunasa taji la Ligi Kuu England na hivyo kuifanya timu hiyo kuifikia Manchester United kwenye rekodi ya kushinda mataji ya ligi, mara 20.

Lakini, Slot anatamba na wachezaji aliowarithi kutoka kwa mtangulizi wake, Jurgen Klopp. Na sasa katika kuanzisha zama zake mpya Anfield, Slot anahitaji mkurugenzi mkuu wa soka, Michael Edwards na mkurugenzi wa michezo Richard Hughes kusajili nyota wapya watakaokuja kufiti kwenye mfumo wa miaka hiyo huku ikifahamu wazi kuna orodha kubwa ya wachezaji wanaweza kuondoka kwenye dirisha lijalo.