Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lionel Messi atia neno sakata la AFCON 2025

Muktasari:

  • Jumanne iliyopita Kamati ya Rufaa ya CAF iliamua kwamba kwa mujibu wa Kifungu cha 84 cha Kanuni za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), Timu ya Taifa ya Senegal imepoteza mechi ya fainali ya fainali hizo iliyochezwa Januari 18, 2026 na matokeo ya mechi hiyo  kuwa ushindi wa mabao 3–0 kwa Morocco.

Mjadala mkali umeendelea kushika kasi kufuatia sintofahamu inayoizunguka michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON 2025), huku wadau wa soka barani Afrika na duniani wakionyesha wasiwasi kuhusu uhalali wa maamuzi yaliyofikiwa katika hatua za mwisho za mashindano hayo.

Jumanne iliyopita Kamati ya Rufaa ya CAF iliamua kwamba kwa mujibu wa Kifungu cha 84 cha Kanuni za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), Timu ya Taifa ya Senegal imepoteza mechi ya fainali ya fainali hizo iliyochezwa Januari 18, 2026 na matokeo ya mechi hiyo  kuwa ushindi wa mabao 3–0 kwa Morocco.

Kanuni ya 82 inafafanua hivi, "Timu itakayoondoka uwanjani kabla ya mchezo kumalizika bila ruhusa ya mwamuzi itapoteza mchezo husika na kuondoshwa kwenye mashindano."

Kanuni ya 84 inafafanua kwamba timu itakayokiuka kifungu cha 82 itapoteza mchezo husika kwa mabao 3:0 ikiwa ni pamoja na kuondoshwa jumla kwenye shindano husika.

Uamuzi huo unafuatia rufaa iliyowasilishwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Morocco (FRMF) kuhusu utekelezaji wa vifungu vya 82 na 84 vya Kanuni za AFCON.

Senegal, ambayo awali ilionekana kunufaika na matokeo ya uwanjani, imeibuka kuwa mstari wa mbele kupinga kile kinachodaiwa kuwa ni ukiukwaji wa haki na taratibu za mashindano.

Katika hali iliyoongeza uzito wa mjadala huo, taarifa zinazosambaa mitandaoni zinadai kuwa nyota wa kimataifa, Lionel Messi, alimtumia ujumbe wa kumtia moyo mshambuliaji wa Senegal, Sadio Mané.

Ujumbe huo, ambao haujathibitishwa rasmi, unamnukuu Messi akimtaja Mané kama “shujaa wa Afrika” na kusisitiza kuwa haki ya Senegal haiwezi kuporwa kirahisi.

Licha ya kutokuwa na uthibitisho wa moja kwa moja, kauli hiyo imepokelewa kwa hisia kali, hasa barani Afrika, ambapo mashabiki wengi wameitafsiri kama ishara ya mshikamano wa kimataifa kwa soka la Afrika na wachezaji wake.