Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Droo Mabingwa Ulaya yadaiwa ni mchongo

UEFA Pict

Muktasari:

  • Droo hiyo ambayo inaendeshwa kwa kompyuta imetoa mechi zinazowafanya baadhi ya mashabiki kuamini kuna kitu kinapangwa.

LONDON, ENGLAND: BAADHI ya mashabiki wa klabu za Ligi Kuu England wanaamini droo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ni kama kuna upangaji wa matokeo baada ya kuhusisha wachezaji kwenda kumenyana na timu zao za zamani kwenye hatua ya kwanza inayochezwa kwa mtindo wa ligi.

Droo hiyo ambayo inaendeshwa kwa kompyuta imetoa mechi zinazowafanya baadhi ya mashabiki kuamini kuna kitu kinapangwa.

Miongoni mwa mechi zilizopangwa kwenye droo hiyo ni ile ya Real Madrid kukipiga na Liverpool huko Anfield, jambo litakalomfanya Trent Alexander-Arnold kurudi kupambana na timu yake ya zamani. Hata hivyo, si yeye pekee wachezaji watakaocheza na timu zao za zamani akiwamo Kevin De Bruyne wa Napoli ambaye atasafiri kurudi Etihad kumenyana na timu yake ya zamani, Manchester City.

Shabiki mmoja aliandika kwenye X: “TAA kucheza dhidi ya Liverpool na KDB vs City. Hebu niambieni, hii haijapangwa kweli.”

Mwingine alikubaliana na hilo, aliposema: “Trent kwenda Anfield, KDB kwenda City, Berta dabi, imepanga hii!?” Shabiki moja wa Liverpool aliibua suala la nyota mpya waliyemnasa dirisha hili, Hugo Ekitike kwamba kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya imempanga atarudi kumenyana na timu yake ya zamani, Eintracht Frankfurt.

Alisema: “Hii kwa asilimia 100 imepangwa, ona Trent atarudi Anfield na Hugo atarudi Frankfurt.”

Arsenal yenyewe itakuwa na kazi ya kumenyana na gwiji wa mahasimu wao, Tottenham, Harry Kane, ambaye kwa sasa anakipiga katika kikosi cha Bayern Munich.

Mechi za kwanza za Ligi ya Mabingwa Ulaya zitafanyika kati ya Septemba 16 na 18.