Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ligi ya Mabingwa Ulaya inavyomwaga pesa kama njugu

MABINGWA Pict

Muktasari:

  • Kuna sababu ya kwa nini klabu nane zilizotumia pesa nyingi zaidi katika dirisha la usajili la 2025 zilitoka Ligi Kuu England, ikiwemo timu zote sita zilizofuzu Ligi ya Mabingw Ulaya kutokana na uhakika huo wa pesa za zawadi.

LONDON, ENGLAND: MKWANJA kamili kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya unaweza kuipa klabu angalau Pauni 115 milioni msimu huu, huku Arsenal, Chelsea, Liverpool na Manchester City zikipata zaidi kutokana na malipo ya televisheni.

Kuna sababu ya kwa nini klabu nane zilizotumia pesa nyingi zaidi katika dirisha la usajili la 2025 zilitoka Ligi Kuu England, ikiwemo timu zote sita zilizofuzu Ligi ya Mabingw Ulaya kutokana na uhakika huo wa pesa za zawadi.

Kiasi cha pesa kinachotolewa katika mashindano mbalimbali ni cha kushangaza na huenda hakuna kinachozidi Ligi ya Mabingwa Ulaya, ambako klabu zinaweza kupata mapato yanayozidi Pauni 100 milioni.

MABI 01

Pesa za zawadi za Ligi ya Mabingwa hufanyaje kazi sasa?

Kama sehemu ya mfumo mpya wa mashindano yao makuu matatu, UEFA ilitangaza mfumo wa mgawanyo wa mapato unaoeleza jinsi jumla ya pesa za zawadi, takribani Pauni 2.88 bilioni, zitakavyogawiwa kila msimu hadi 2026/27.

Zaidi kidogo ya Pauni 2.1 bilioni (74.38%) zitasambazwa kwa klabu zinazoshiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya na Super Cup, Pauni 490.7 milioni (17.02%) kwa timu zinazoshiriki Europa League na Pauni 247.5 milioni (8.6%) kugawiwa kwa Europa Conference League.

Katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, fungu hilo linagawanywa zaidi kama ifuatavyo;


1) Mgao sawa (Pauni 581.7milioni / 27.5%)

Ada ya kuanzia ya Pauni 16.2 milioni kwa kila moja ya klabu 36 zinazofuzu awamu ya ligi. Kiasi hiki kinahakikishwa bila kujali matokeo yao baadaye kwenye mashindano.


2) Malipo yanayotegemea matokeo (Pauni 793.6 milioni / 37.5%)

Pauni 1.8 milioni kwa kila ushindi katika mechi hizo za awamu ya ligi. Pauni 608,000 itatolewa kwa kila mechi ya sare, huku Pauni 238,000 italipwa kwa timu itakayoshika nafasi ya mwisho katika awamu hiyo ya ligi.

Malipo ya nafasi huongezeka hatua kwa hatua, kuanzia timu ya 36 ikipata Pauni 238,000 hadi timu ya kwanza ikipata Pauni 8.57 milioni.

Pesa ambazo hazijasambazwa kutokana na sare (kila sare ina thamani ya Pauni 608,000) huongezwa kwenye malipo ya nafasi mwishoni mwa awamu ya ligi, hivyo kiasi halisi cha pesa kwa nafasi huwa kikubwa zaidi. Pia kuna pesa za ziada kwa kumaliza ndani ya nane bora na kwa kumaliza kati ya nafasi ya 9 hadi 16.

Hivi ndivyo Liverpool ilivyopata pesa nyingi licha ya kutolewa katika hatua ya 16 bora msimu uliopita.


3) Nguzo ya thamani (Pauni 740.6 milioni / 35%)

Hii ni mchanganyiko wa malipo kulingana na; Viwango vya mgawo wa klabu (club coefficient) na mapato ya televisheni (TV pool).

Hii ni ngumu kuhesabu kwa usahihi, lakini kwa kawaida huwazawadia klabu kubwa na za kihistoria zaidi. Paris Saint-Germain, Bayern Munich, Real Madrid na klabu nne za mara kwa mara za England (Man City, Liverpool, Chelsea na Arsenal) vinanufaika zaidi, huku Qarabag, Pafos na Kairat vikitarajiwa kupata kiasi kidogo zaidi.

Makadirio ya malipo ya nguzo ya thamani kwa klabu zote 36 yatajumlishwa kwenye pesa za mwisho za zawadi na kwa klabu chache jumla inaweza kuvuka Pauni 100 milioni.

Pia kuna ada ya kudumu ya Pauni 3.73 milioni kwa klabu zote zinazotolewa kwenye mechi za mchujo kabla ya awamu ya ligi kuanza kwa klabu kama Celtic na Rangers.

MABI 03

Kila timu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya tayari imepata pesa kiasi gani?

Ifuatayo ni makadirio ya kiasi cha pesa ambazo kila timu tayari imepata katika Ligi ya Mabingwa Ulaya katika msimu huu wa 2025/26, kabla ya mapato ya siku ya mechi na mambo mengine kuzingatiwa.

Bayern Munich – Pauni 85.76 milioni (imefuzu 16 bora)

Man City – Pauni 83.41 milioni (16 bora)

Liverpool – Pauni 83.28 milioni (16 bora)

Arsenal – Pauni 82.59 milioni (16 bora)

Chelsea – Pauni 78.91 milioni (16 bora)

Barcelona – Pauni 76.23 milioni (16 bora)

Tottenham – Pauni 71.86 milioni (16 bora)

PSG – Pauni 70.83 milioni  (mchujo wa mtoano)

Real Madrid – Pauni 69.55 milioni (mchujo wa mtoano)

Borussia Dortmund – Pauni 60.39 milioni (mchujo)

Inter – Pauni 60.82 milioni (mchujo)

Atletico Madrid – Pauni 59.69 milioni (mchujo)

Sporting – Pauni 55 milioni (16 bora)

Bayer Leverkusen – Pauni 59.74 milioni (mchujo)

Juventus – Pauni 54.21 milioni (mchujo)

Atalanta – Pauni 51.82 milioni (mchujo)

Monaco – Pauni 47.8 milioni (mchujo)

Benfica – Pauni 46.57 milioni (mchujo)

Newcastle – Pauni 46.44 milioni (mchujo)

Marseille – Pauni 46.17 milioni (imetolewa awamu ya ligi)

Eintracht Frankfurt – Pauni 42.21 milioni

Club Brugge – Pauni 41.33 milioni

Napoli – Pauni 41.16 milioni

Olympiacos – Pauni 39.39 milioni

Villarreal – Pauni 39.31 milioni

PSV – Pauni 39.03 milioni

Ajax – Pauni 37.23 milioni

Bodoe/Glimt – Pauni 36.22 milioni

Athletic Bilbao – Pauni 33.41 milioni

Galatasaray – Pauni 33.28 milioni

FC Copenhagen – Pauni 32.53 milioni

Qarabag – Pauni 30.89 milioni

Union Saint-Gilloise – Pauni 28.15 milioni

Slavia Prague – Pauni 26.26 milioni

Pafos – Pauni 26.13 milioni

Kairat – Pauni 18.43 milioni

MABI 02

Kiasi gani cha pesa bado kinaweza kupatikana?

Awamu ya ligi ilikuwa na faida kubwa sana, ikiwa na pesa kwa ushindi, sare na nafasi ya mwisho.

Kulikuwa na Pauni 1.74 milioni kwa kumaliza ndani ya nane bora. Pauni 868,000 kwa kumaliza kati ya nafasi ya 9–16. Hiyo ina maana, kila nafasi ya ligi ilikuwa na thamani ya Pauni 238,000, ikiongezeka hadi nafasi ya kwanza kupata Pauni 8.57 milioni.

Mbali na malipo ya awamu ya ligi, kuna pesa kubwa kwa kusonga mbele:

Kufuzu mchujo wa mtoano – Pauni 868,000

Hatua ya 16 bora – Pauni 9.55 milioni

Robo fainali – Pauni 10.85 milioni

Nusu fainali – Pauni 13.02 milioni

Washindi wa pili – Pauni 16.06 milioni

Mabingwa – Pauni 21.7 milioni

Kufuzu fainali ya Super Cup kunalipa Pauni 3.47 milioni na ushindi unaongeza Pauni 868,000 zaidi.

Kwa hiyo, kushinda kila mchezo wa awamu ya ligi na hatimaye kutwaa taji kungeingiza angalau Pauni 115.56 milioni, kabla ya pesa za TV na mgawo kuhesabiwa. Ni mkwanja mrefu kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya.