Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kylian Mbappe ni rekodi juu ya rekodi

KYLIAN Pict

Muktasari:

  • Cha kushangaza zaidi, tangu mwaka 2018, Mbappe amefunga mabao mengi zaidi katika hatua za mtoano za Kombe la Dunia (11) kuliko timu za Brazil (10), England (10), Ureno (9) na Hispania (4).

PHILADELPHIA, MAREKANI: KYLIAN Mbappe sasa amebakiwa na bao moja tu kufikia rekodi ya Lionel Messi katika orodha ya wafungaji bora wa muda wote wa Kombe la Dunia, baada ya kufikisha mabao 19 katika michezo 19 ya mashindano hayo.

Cha kushangaza zaidi, tangu mwaka 2018, Mbappe amefunga mabao mengi zaidi katika hatua za mtoano za Kombe la Dunia (11) kuliko timu za Brazil (10), England (10), Ureno (9) na Hispania (4).

Mbappe ameyafanya hayo yote katika mchezo wa hatua ya 16 bora ya Kombe la Dunia 2026 katika ushindi wa bao 1-0 ilioupata Ufaransa dhidi ya Paraguay, Jumamosi Julai 4, 2026.

Mchezo huo ulionekana kuwa wa kukatisha tamaa kwa Ufaransa na nahodha wao, Mbappe, kwani walishindwa kupiga shuti lolote lililolenga lango katika kipindi cha kwanza.

KYLI 05

Joto kali lilikuwa na athari kubwa, huku mechi hiyo ikiingia kwenye rekodi ya moja ya michezo yenye joto kali zaidi kuwahi kuchezwa katika Kombe la Dunia. Wakati wa kuanza kwa mchezo, kiwango cha joto kilisajiliwa kuwa nyuzi joto 38.3°C kwa mujibu wa ukurasa rasmi wa National Weather Service.

Rekodi ya mchezo wenye joto kali zaidi katika Kombe la Dunia ni nyuzi 43°C, wakati Jamhuri ya Ireland ilipocheza dhidi ya Mexico huko Florida mwaka 1994.

Hata hivyo, Ufaransa ilipata njia ya kushinda licha ya joto kali pamoja na mbinu ngumu za Paraguay.

"Tunajua kucheza mpira mbaya pia," Mbappe amesema baada ya mchezo.

"Wao (Paraguay) walidhani tungekuja kwa suti za kifahari, lakini tulikuwa tayari. Hata katika mchezo huo tulikuwa bora kuliko wao.

KYLI 04

"Huo ndiyo mtindo wao wa soka. Hakuna njia sahihi au isiyo sahihi ya kucheza mpira. Walijaribu kutushinda kwa njia hiyo, lakini sisi ndio tuliibuka washindi."

Kocha wa Ufaransa, Didier Deschamps, ambaye sasa amekuwa kocha wa kwanza kufikisha ushindi wa kumi katika hatua za mtoano za Kombe la Dunia, amesema aliwaagiza wachezaji wa kikosi hicho kumlinda Mbappe katika dakika za mwisho wakati Paraguay wakisaka bao la kusawazisha.

KYLI 03

"Niliwaambia wachezaji wawili wakubwa zaidi waende wakasimame karibu na Kylian mwishoni mwa mchezo kwa sababu walikuwa wanataka kumuangusha kwa makusudi," amesema Deschamps.

"Haikuwa rahisi. Wanatumia kila mbinu inayowezekana. Si aina ya soka itakayowavutia mashabiki kuja uwanjani, lakini walijilinda vizuri. Daima ni vigumu kucheza dhidi ya timu za Amerika Kusini."

Mbappe alilengwa tangu mwanzo wa mchezo lakini alibaki mtulivu na alijibu uchokozi wa Paraguay kwa kucheka na kupuuza mbinu zao uwanjani.

KYLI 02

"Nimependa jinsi Mbappe alivyojiendesha katika mchezo huu," amesema kipa wa zamani wa England na Manchester City, Joe Hart.

"Wachezaji wa Paraguay walimfuata tangu dakika ya kwanza. Alipokuwa anawacheka, alikuwa na haki ya kuonyesha kujiamini.

"Mimi binafsi nisingependa kucheza soka la aina hiyo. Mwamuzi pia hakusaidia kwa hali yoyote. Ukweli ni kwamba hakuna hata mchezaji mmoja wa Paraguay aliyeonyeshwa kadi ndani ya dakika 90, ni jambo la kushangaza."

Kiungo wa zamani wa Ujerumani, Thomas Hitzlsperger, amesema hana heshima yoyote kwa Paraguay kutokana na namna walivyocheza.

KYLI 01

"Kama wewe ni Mparaguay, huenda unaipenda timu yako kwa sababu wanapambana kama mashujaa," amesema.

"Lakini kama wewe ni Mfaransa au shabiki asiyeegemea upande wowote, huwezi tena kuwaheshimu. Hili si jambo la aibu tu, ni baya zaidi ya hapo."