Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kumbe Van Dijk anabaki Anfield

VAN Pict

Muktasari:

  • Van Dijk ambaye mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu huu pamoja na Mohamed Salah na Trent Alexander-Arnold ni miongoni mwa wachezaji wanaotajwa kuwa wataondoka mwisho wa msimu huu. 

LIVERPOOL, ENGLAND: BEKI kisiki na nahodha wa Liverpool, Virgil van Dijk ameweka wazi kwamba yupo karibu kusaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia katika viunga hivyo kwa muda mrefu zaidi.

Van Dijk ambaye mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu huu pamoja na Mohamed Salah na Trent Alexander-Arnold ni miongoni mwa wachezaji wanaotajwa kuwa wataondoka mwisho wa msimu huu. 

Hata hivyo, beki huyo amefichua kuwa kwa sasa kuna mazungumzo chanya yanayoendelea kati ya wawakilishi wake na mabosi wa Liverpool hivyo ana asilimia kubwa za kubaki.

“Kuna maendeleo mazuri katika mazungumzo, siwezi kusema kama nitaondoka au nitabaki, tutaona baada ya mazungumzo haya ya ndani,” alisema Van Dijk alipoulizwa juu ya hatima yake katika kikosi cha majogoo hao wa Jiji la Liverpool.

Van Dijk, 33, amekuwa mmoja kati ya wachezaji tegemeo wa Liverpool tangu ajiunge nao mwaka 2018 kwa ada ya uhamisho ya Pauni 75 milioni kutoka Southampton.

Liverpool ipo kileleni ikiwa na  pointi 73,  huku mkononi ikiwa imebakiza mechi saba na tofauti ya alama kati yake na Arsenal iliyo nafasi yapili ni pointi 11 tu. Ilishindwa kuongeza pengo la alama wikiendi iliyopita baada ya kukubali kichapo cha mabao 3-2 ambapo katika dakika 14 za mwanzo wa mchezo huo, Liverpool iliruhusu mabao matatu ya haraka.

Van Dijk ameongeza kwa kusema kwamba mechi hiyo walipoteza kwa kutokuwa makini lakini wanatazamia mechi za mbele ambazo wana imani kubwa kwamba watashinda na kutangaza ubingwa mapema ambapo itatakiwa kushinda mechi nne ili kutwaa taji hilo.