Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kombe la Dunia linaweza kuondoka Marekani? IKO HIVI

DUNIA Pict

Muktasari:

  • Vilevile, wadau wengi kutoka Ulaya wametaka Marekani iondolewe uandaaji baada ya  Trump kuitaka Denmark kukabidhi eneo la Greenland kwa Marekani kwa kile alichodai kuwa ni sababu za kiusalama.

NEW YORK, MAREKANI: SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (FIFA) linaweza kuwa na uwezo wa kuiondolea Marekani haki ya kuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia la FIFA 2026, ikiwa moja kati ya vipengele katika mkataba wa makubaliano kitakiukwa.

Wakati siku zikizidi kukatika kabla ya kuanza kwa Kombe la Dunia la FIFA 2026, waandaaji wa michuano hiyo tayari wameshaanza kufanya kazi katika miji 18 itakayokuwa mwenyeji ambayo ni Atlanta, Boston, Dallas/Arlington, Houston, Kansas City, Los Angeles, Miami, New York/New Jersey, Philadelphia, eneo la Ghuba ya San Francisco, Seattle, Toronto, Vancouver, Mexico City, Guadalajara na Monterrey.

Hata hivyo, kumekuwepo na wito kutoka kwa wabunge, wanahabari na mashabiki wakiitaka Marekani iondolewe haki ya kuwa mwenyeji kutokana na hali ya sasa ya kisiasa chini ya rais wao Donald Trump.

Januari mwaka huu, kundi la wabunge 23 wa Uingereza lilisaini azimio linalozitaka taasisi za michezo za kimataifa kuiondolea Marekani haki ya kuandaa mashindano mbalimbali ikiwamo Kombe la Dunia.

Jambo hilo lilichangiwa na hali ya kisiasa iliyopo katika nchi hiyo tangu Trump aingie madarakani Januari 2025.

Mashabiki wengi wamekuwa na wasiwasi wa hata kupata viza baada kuongezeka kwa masharti katika miezi ya hivi karibuni, pia kumekuwapo kwa operesheni kali inayofanywa na Idara ya Uhamiaji ya Marekani (ICE).

Vilevile, wadau wengi kutoka Ulaya wametaka Marekani iondolewe uandaaji baada ya  Trump kuitaka Denmark kukabidhi eneo la Greenland kwa Marekani kwa kile alichodai kuwa ni sababu za kiusalama.

Watu wengi wamekuwa wakiendesha kampeni za kutaka Marekani inyang’anywe uandaaji lakini je, FIFA ina mamlaka ya kufanya hivyo?

Kitaalamu, inaelezwa kuwa ndiyo, FIFA inaweza kufanya hivyo, lakini si kirahisi.

Kwa mujibu wa kanuni za Kombe la Dunia 2026, FIFA ina haki ya “kufuta, kupanga upya au kuhamisha mechi moja au zaidi (au Kombe la Dunia la FIFA 2026 lote) kwa sababu kadhaa ikiwamo nguvu au mtazamo wa wengi (vyama vya soka vinavyoshiriki), masuala ya afyac(milipuko ya magonjwa hatarishi na sababu za kiusalama au ulinzi.”

Akizungumza katika mahojiano maalum na tovuti ya SPORTbible, Jack Anderson, Profesa wa Sheria ya katika masuala ya Michezo katika Chuo Kikuu cha Melbourne, alieleza kuwa kuiondolea Marekani haki ya kuwa mwenyeji ni “jambo gumu ingawa bado linaweza kutokea.”