Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Newcastle United atoa mpya dili la Isak

KOCHA Pict

Muktasari:

  • Howe pia amesisitiza kwamba uamuzi wowote utakaofanywa juu ya hatma ya staa huyo lazima uwe ni kwa maslahi ya klabu.

NEWCASTLE, ENGLAND: KOCHA wa Newcastle United, Eddie Howe amekiri kuwa timu hiyo inapaswa kufanya uamuzi juu ya mustakabali wa staa wao Alexander Isak ambaye ameweka wazi kuwa anataka kuondoka katika dirisha hili.

Howe pia amesisitiza kwamba uamuzi wowote utakaofanywa juu ya hatma ya staa huyo lazima uwe ni kwa maslahi ya klabu.

Isak ambaye anakadiriwa kuuzwa kwa Pauni 150 milioni tayari ameshawaeleza viongozi wa Newcastle kuwa anataka kuondoka katika dirisha hili na hatasaini mkataba mpya baada ya mkataba wake wa sasa kumalizika mwaka 2028.

Fundi huyu, mwenye umri wa miaka 25, hakuwa sehemu ya kikosi kilichosafiri kwenda Asia kwa ziara ya maandalizi ya msimu mpya kwa kile kilichoripotiwa kuwa ni majeraha ya paja.

Gazeti la Sunsport limeeleza kuwa klabu ya Al-Hilal ya Saudi Arabia imempa ofa ya mshahara wa Pauni 32 milioni kwa mwaka lakini amekataa kwa sababu  moyo wake uko Liverpool.

Alipoulizwa kuhusu mustakabali wa Isak saa chache baada ya kutua Singapore ambako Newcastle imeweka kambi ya maandalizi ya msimu mpya, kocha Howe alisema:

"Bila shaka kuna mambo yanayoendelea nyuma ya pazia. Isak atakuwa anayajua, kila siku anatajwa kwenye vyombo vya habari na nina uhakika si jambo jepesi kwa mtu yeyote kuwa katika hali kama hiyo.

Mimi binafsi sipo katika mawasiliano ya kila siku na mtu yeyote wa bodi. Masuala ya usajili yanashughulikiwa na watu waliobaki nyumbani. Niko na wachezaji 30 hapa ninaowajibika kuwaangalia na kuandaa timu kwa ubora wote tunaoweza.

Ninachofahamu kwa sasa hakuna mazungumzo kuhusu mkataba mpya lakini tuna uhusiano mzuri sana naye. Amekuwa bora sana kwetu tangu alipojiunga. Anapendwa sana kwenye chumba cha kubadilishia nguo.

Tungependa aendelee na safari yake hapa Newcastle. Tunatumai atavaa tena jezi ya rangi nyeusi na nyeupe, hiyo ndiyo tunayotaka kuiona."

"Lakini daima kuna uamuzi mkubwa ya kufanya ukiwa Newcastle. Hilo ni jambo la kawaida kwa klabu kama hii. Siwezi kuweka muda maalum wa lini kila kitu kitakuwa sawa kuhusu hatma yake, lakini ni lazima uwe uamuzi sahihi kwa ajili ya klabu. Lengo kuu ni kuisogeza klabu mbele kwa njia yoyote ile. Hicho ndicho tunachojaribu kukifanya, bila kujali hali ya Alex. Bila shaka, tunataka utulivu na tunataka kikosi kiwe  na mshikamano mzuri. Tupo katika nafasi nzuri kifedha. Tumejipanga kufanikiwa."