Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Argentina yajipa matumaini Kombe la Dunia 2026

MATUMAINI Pict (1)

Muktasari:

  • Video zilizosambaa zimemuonyesha Bellingham akishika bega lake la kushoto huku akionekana kuumia baada ya ushindi dhidi ya Norway.

LOS ANGELES, MAREKANI: VYOMBO vya habari nchini Argentina vinaamini nyota wa England, Jude Bellingham, huenda akawa na majeraha kabla ya mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Dunia dhidi ya Argentina.

Video zilizosambaa zimemuonyesha Bellingham akishika bega lake la kushoto huku akionekana kuumia baada ya ushindi dhidi ya Norway.

Hata hivyo, taarifa zinaeleza kuwa kiungo huyo amekuwa akisumbuliwa na tatizo hilo tangu alipoumia akiwa Real Madrid mwaka 2025 kabla ya kufanyiwa upasuaji.

JAMBO Pict

Licha ya hali hiyo, Bellingham anatarajiwa kuanza dhidi ya Argentina akiwa tayari amefunga mabao sita katika mashindano hayo.

Baada ya ushindi dhidi ya Norway, Bellingham pia alionekana kutofautiana kimtazamo na kocha Thomas Tuchel kuhusu namna England ilivyocheza, akisisitiza kuwa ushindi ndiyo jambo muhimu zaidi katika hatua hiyo ya mashindano.

KAN 01
KAN 01

Huyu amekuwa mmoja kati ya wachezaji muhimu kwenye kikosi cha England kutokana na kiwangp chake ambacho amekuwa akikionyesha kwenye michezo aliyocheza hadi sasa.

England itaavaana na Argentina kwenye mchezo mkali wa hatua ya nusu fainali leo baada ya jana Ufaransa kuvaana na Hispania kwenye mechi nyingine iliyokuwa na msisimko mkubwa.

Hata hivyo, vyombo vya habari vya England vimesema kuwa mchezaji huyo yupo fiti kwa ajili ya mchezo huo wenye matumaini makubwa kwao.