Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Man United afunguka tatizo la Mainoo

MAINOO Pict

Muktasari:

  • Kiungo huyo amekuwa akipewa dakika chache sana za kucheza kwenye kikosi cha miamba hiyo ya Old Trafford msimu huu baada ya Man United kumaliza kwenye nafasi ya 15 kwenye Ligi Kuu England msimu uliopita.

MANCHESTER, ENGLAND: KOCHA, Ruben Amorim amekiri kwamba kufeli kwa Manchester United kufuzu michuano ya Ulaya na kutupwa nje mapema katika Kombe la Ligi kumesababisha madhara makubwa kwa kiungo Kobbie Mainoo.

Kiungo huyo amekuwa akipewa dakika chache sana za kucheza kwenye kikosi cha miamba hiyo ya Old Trafford msimu huu baada ya Man United kumaliza kwenye nafasi ya 15 kwenye Ligi Kuu England msimu uliopita.

Mainoo, 20, hajaanzishwa kwenye mechi yoyote ya ligi hadi sasa msimu huu na aliishia tu kwenye benchi katika mechi iliyopita dhidi ya Nottingham Forest. Staa huyo ambaye ni zao la kutokea kwenye akademia ya Man United amekuwa na wakati mgumu wa kupata nafasi ya kucheza chini ya kocha Amorim tofauti na ilivyokuwa awali tangu alipoibukia katika msimu wa 2023/24, ambapo kiwango chake kilimpa nafasi ya kuitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya England.

Mainoo aligomea kuondoka kwa mkopo katika dirisha lililopita la majira ya kiangazi, lakini kwa sasa amekuwa tu wa ziada kwenye kikosi hicho cha Man United ambapo kwa wiki kinacheza mechi moja tu. Kitendo cha kutolewa mapema kwenye Kombe la Ligi kumekuwa na athari kubwa kwa wachezaji wengine kupata nafasi ya kucheza.

Na kocha Amorim amekiri kwamba kiwango cha Mainoo mazoezini ni kizuri kiasi cha kutosha kupewa nafasi ya kuanza kwenye mechi, lakini shida ni nafasi hiyo kupatikana kutokana na Bruno Fernandes na Casemiro kuwa chaguo la kwanza kwenye eneo la kiungo.

"Naona jinsi Kobbie Mainoo anavyofanya mazoezini, anastahili kucheza, lakini ndiyo hivyo kuna mtu lazima awe nje na anacheza vizuri. Tulipaswa kuwapo kwenye Kombe la Ligi kwasababu nataka kumwona Kobbie Mainoo akicheza, nataka kumwona Josh, wote hawa wanastahili kucheza, lakini mechi ni moja, hivyo unahitaji kufanya uchaguzi," amesema Amorim.