Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Liverpool afichua kilichomsibu Alexander Isak 

ISAK Pict

Muktasari:

  • Liverpool ilionyesha ubabe dhidi ya wenyeji wao baada ya kufungwa bao la mapema, huku wachezaji watano tofauti wakifunga mabao yaliyohakikisha kikosi cha Merseyside kinaondoka na ushindi na kusitisha matokeo mabaya yaliyowaandama kwa siku za karibuni.

Kocha wa Liverpool, Arne Slot amefichua sababu za mshambuliaji Alexander Isak kushindwa kuendelea na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Eintracht Frankfurt ya Ujerumani iliyokubali kipigi cha 5-1, usiku wa Oktoba 22, 2025.

Liverpool ilionyesha ubabe dhidi ya wenyeji wao baada ya kufungwa bao la mapema, huku wachezaji watano tofauti wakifunga mabao yaliyohakikisha kikosi cha Merseyside kinaondoka na ushindi na kusitisha matokeo mabaya yaliyowaandama kwa siku za karibuni.

Isak ambaye alijiunga na Liverpool msimu huu akitokea Newcastle United, hakuwa sehemu ya kikosi cha Arne Slot baada ya mapumziko, hali ambayo ilizua maswali kwa baadhi ya mashabiki waliokuwa wanafuatilia mchezo huo.

ISA 01

Kocha Slot ametoa ufafanuzi kwa nini mshambuliaji huyo hakuonekana kikosini wakati kikosi chake kikirejea uwanjani kwa ajili ya kipindi cha pili cha mtanange huo, uliopigwa kwenye dimba Deutsche Bank Park.

Kocha huyo raia wa Uholanzi, amesema, Isak alishindwa kuendelea na mechi hiyo kutokana na majeraha madogo ya nyonga, ambayo aliyapata katika kipindi cha kwanza cha mchezo, hivyo madaktari walishauri ampumzishe kwa kuhofia huenda angepata maumivu zaidi.

“Alex (Isak) ilibidi atoke wakati wa mapumziko kwa sababu alihisi maumivu kidogo kwenye nyonga. Kwa bahati mbaya ilibidi atoke, kwa hivyo tuombe mambo yaende vizuri. Si rahisi hasa kwa mchezaji ambaye amekuwa nje kwa muda mrefu.”

ISA 02

Kocha huyo wa Liverpool alikuwa akizungumzia maandalizi ya msimu wa Isak yaliyokatizwa akiwa na klabu yake ya zamani Newcastle United, ambapo mshambuliaji huyo raia wa Swden alilazimika kuingia kwenye mfumo wa Liverpool, kwa siku kadhaa baada ya kukamilisha taratibu wa uhamisho wake.

Hata hivyo, majeraha ya nyonga si jambo jipya kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, kwani amewahi kukumbwa na tatizo hilo mara kadhaa akiwa na Newcastle United.

Kutokana na hali hiyo, huenda Isak akawa na wakati mgumu wa kupambana na muda ili kuwa fiti kwa mchezo wa Jumamosi, Oktoba 25, 2025 dhidi ya Brentford.