Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha EPL asema Man United hatari, atoa onyo

KOCHA Pict

Muktasari:

  • Mabao kutoka kwa Rasmus Hojlund, Patrick Dorgu, Amad Diallo na Ethan Williams yaliiweka Man United mbele kwa 4-0 kabla ya Matthijs de Ligt kujifunga na kuipa Bournemouth bao la kufutia machozi kwenye Uwanja wa Soldier Field uliokuwa na mvua nyepesi.

LONDON, ENGLAND: KOCHA wa Bournemouth, Andoni Iraola amezionya klabu za Ligi Kuu England kuwa Manchester United ni “timu kali sana” baada ya kushuhudia kikosi hicho cha mashetani wekundu kikiiadhibu timu yake mabao 4-1 Jumatano ya wiki katika mchezo wa kirafiki uliopigwa jijini Chicago.

Mabao kutoka kwa Rasmus Hojlund, Patrick Dorgu, Amad Diallo na Ethan Williams yaliiweka Man United mbele kwa 4-0 kabla ya Matthijs de Ligt kujifunga na kuipa Bournemouth bao la kufutia machozi kwenye Uwanja wa Soldier Field uliokuwa na mvua nyepesi.

Huu ulikuwa ushindi wa pili mfululizo kwa Manchester United ambayo inaonekana kuamka upya katika maandalizi ya msimu huu baada ya kumaliza nafasi ya 15 kwenye Ligi Kuu msimu uliopita.

Akizungumza baada ya mechi, kocha wa Bournemouth, Iraola, alisifu kikosi cha Amorim na kukiri: “Kwa sasa levo yetu ipo chini sana tofauti na Man United. Nadhani Man United ni timu kali sana na imefanya usajili mzuri,” alisema Mhispania huyo alipofanya mahojiano kupitia Sky Sports News.

“Leo wameonyesha wako juu yetu kwa sasa, na hicho ndicho kinachoonekana, bado tunao muda wa kujiandaa. Tunahitaji kubadilika na kuendelea kujiandaa kwa msimu.”

Bournemouth imekuwa na maandalizi yenye matokeo mchanganyiko hadi sasa, ambapo kichapo kizito kutoka kwa United kinakuja siku chache tu baada ya kupata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Everton.

Matokeo ya mechi hiyo  yanaweza kuwatia hofu mashabiki wa Bournemouth, hasa ikizingatiwa kuwa Man United iliwakosa nyota wao wapya Matheus Cunha na Bryan Mbuemo.

Mashabiki wa  Man United bado hawajawaona wawili hao wakicheza pamoja kwani Mbuemo bado yuko kwenye mchakato wa kurudi kwenye kiwango kamili cha mwili huku Cunha akipumzishwa kutokana na uchovu.

Uongozi wa Man United umetumia karibu Pauni 140 milioni kuwasajili washambuliaji hao wakitumaini wataongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji ambayo ilikuwa dhaifu msimu uliopita.

Licha ya kusajiliwa kwa wachezaji hao wawili, kocha Ruben Amorim bado anataka kuimarisha safu yake ya ushambuliaji na sasa inahusishwa na nyota wa RB Leipzig, Benjamin Sesko, kama chaguo lao la kwanza la mshambuliaji.