Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha England kuwaweka kitako mastaa wake

TUCHEL Pict

Muktasari:

  • Kocha Tuchel, ambaye hatakuwa na mechi nyingine yoyote hadi Machi mwakani, atatumia wiki kadhaa zijazo kuzungumza na mastaa wake kwa simu za video au mazungumzo ya ana kwa ana ili kuwekana sawa kabla ya fainali hizo kuanza.

LONDON, ENGLAND: KOCHA mkuu wa England, Thomas Tuchel amepanga kuzungumza na mastaa wake takriban 60 ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kikosi chake kitakachokwenda kwenye fainali za Kombe la Dunia 2026.

Kocha Tuchel, ambaye hatakuwa na mechi nyingine yoyote hadi Machi mwakani, atatumia wiki kadhaa zijazo kuzungumza na mastaa wake kwa simu za video au mazungumzo ya ana kwa ana ili kuwekana sawa kabla ya fainali hizo kuanza.

Tuchel, ambaye amefanya kazi na wachezaji zaidi ya 50 kwenye uteuzi wa kikosi chake, alithibitisha atapanda ndege kwenda Madrid kuzungumza na mastaa Jude Bellingham na Trent Alexander-Arnold.

Kocha huyo Mjerumani anataka kuweka mambo sawa na Bellingham juu ya tabia yake baada ya kurusha mkono wakati alipofanyiwa mabadiliko wakati England ilipoichapa Albania 2-0 katika mechi ya mwisho kufuzu Kombe la Dunia 2026.

TUCH 01

Tuchel atazungumza na Alexander-Arnold, ambaye kwa sasa hapati nafasi kwenye kikosi cha kwanza. Katika mechi ya Tirana, kocha huyo wa Three Lions, alimwanzisha beki wa zamani wa Liverpool, Jarell Quansah, ambaye kwa sasa anakipiga Bayer Leverkusen, katika beki ya kulia licha ya kwamba yeye ni beki wa kati.

Tuchel amesema: “Kwanza, kazi yangu sasa itakuwa kuwasiliana na kila mmoja, wachezaji kama Trent. Wachezaji waliopo kwenye orodha yetu ni 55 hadi 60, kuwafikia, kuwasiliana nao, kujadili nao kila kitu. Kuwaaambia kitu gani cha kufanya, waboreshe wapi.

Hiyo ndiyo kazi yangu kwa wiki zijazo na miezi ijayo.”

TUCH 02

Vikosi vya Kombe la Dunia viliongezwa kutoka wachezaji 23 hadi 26 kwenye fainali za Kombe la Dunia 2022 huko Qatar, hivyo kuna uhakika mkubwa Fifa itaendelea na utaratibu huo. Droo ya makundi ya Kombe la Dunia itapangwa huko Washington, Desemba 5 na England itakuwa na mechi mbili za kirafiki dhidi ya Japan na Uruguay, Machi mwakani.

Kisha itacheza mechi mbili za kirafiki huko Florida kabla ya kuanza kwa fainali hizo za Kombe la Dunia 2026.