Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tuchel atuma ujumbe kwa mastaa England

Muktasari:

  • Bosi wa kikosi cha Three Lions, Tuchel alikiri kwamba kuna mastaa kadhaa wataanzia benchini kwenye fainali hizo za Amerika, lakini amewataka kukubaliana na hali hiyo, ili wakati watakapoingizwa wahakikishe wanakuwa moto wanapopata nafasi ya kucheza.

LONDON, ENGLAND: KOCHA mkuu wa England, Thomas Tuchel amewataka mastaa wake watakaoanzia benchini kwenye fainali za Kombe la Dunia kuwa na hasira wanapoingia uwanjani ili kunyakua taji hilo.

Bosi wa kikosi cha Three Lions, Tuchel alikiri kwamba kuna mastaa kadhaa wataanzia benchini kwenye fainali hizo za Amerika, lakini amewataka kukubaliana na hali hiyo, ili wakati watakapoingizwa wahakikishe wanakuwa moto wanapopata nafasi ya kucheza.

Katika kuelekea mechi yao ya mwisho ya kufuzu fainali hizo za Kombe la Dunia dhidi ya Albania, Tuchel alisema: “Ni wazi wachezaji watachukia kwa kuanzia benchini. Lakini, kama ukitazama timu zilizoshinda michuano, ilipata nguvu kubwa kwa wachezaji wao wa benchini. Kila mtu lazima apambane hata wakati ambao ataingia kutokea benchini.”

Tuchel hataanzisha mastaa wake wote kwenye fainali hizo za mwakani, ambapo wakali wengine kama Phil Foden na Cole Palmer wanaweza kuanzia benchini ili kuja kubadili mchezo watakapoingizwa.

Mpango wake mwingine pia ni kufanya mabadiliko wakati wa mapumziko kutokana na hali ya joto ya huko Marekani, hasa ikizingatiwa kwamba wachezaji wanaopaswa kubadilishwa ni watano tu na hiyo ifanyike kwa awamu tatu ndani ya mchezo.

Tuchel alisema: “Lazima tufikirie hilo kwenye mapana makubwa na pengine unaweza kutumia fursa ya kubadili wakati wa mapumziko. Tunaweza kufanya mabadiliko ya mchezaji mmoja au wawili wakati wa mapumziko kabla ya kutumia nafasi nyingine kwenye kipindi cha pili.”