Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Aston Villa afichua ishu ya Martinez

EMERY Pict

Muktasari:

  • Kipa Martinez mara nyingi amekuwa akivaa kitambaa cha unahodha wa Aston Villa katika mechi ambazo nahodha mkuu John McGinn hachezi, lakini haikuwa hivyo usiku wa Alhamisi iliyopita wakati timu hiyo ilipokipiga na Maccabi Tel-Aviv.

BIRMINGHAM, ENGLAND: KOCHA wa Aston Villa, Unai Emery amethibitisha kwamba kipa Emi Martinez kwa sasa si nahodha msaidizi tena wa kikosi hicho cha Villa Park baada ya kuvuliwa kitambaa hicho kufuatia mchakato wake wa kulazimisha kuachana na timu hiyo kwenye dirisha lililopita.

Kipa Martinez mara nyingi amekuwa akivaa kitambaa cha unahodha wa Aston Villa katika mechi ambazo nahodha mkuu John McGinn hachezi, lakini haikuwa hivyo usiku wa Alhamisi iliyopita wakati timu hiyo ilipokipiga na Maccabi Tel-Aviv.

Katika mchezo huo, staa wa kimataifa wa England, Ezri Konsa, ndiye aliyekuwa amevaa kitambaa cha unahodha wa kikosi cha Aston Villa.

Kipa Martinez alikuwa kwenye mchakato wa kuachana na Villa Park kwenye dirisha lililopita la majira ya kiangazi wakati Manchester United, iliyokuwa ikitafuta kipa mpya kuhusishwa nayo.

Baada ya kukwama kwa dili hilo la kutua Old Trafford, kipa Martinez aliwekwa kando kwenye mechi za kwanza na kocha Emery huko Aston Villa kabla ya kuondolewa kwenye hadhi ya kuwa nahodha msaidizi wa kikosi hicho cha Ligi Kuu England.

Emery alithibitisha hilo Alhamisi kwamba Martinez si nahodha tena msaidizi, aliposema: "Nahodha mkuu ni John McGinn. Tutaamua kwa jinsi tulivyo na tutatazama nani atakuwa nahodha mwingine. Kwa kawaida, tulikuwa na nahodha namba mbili, Emi Martinez, lakini sasa ni Konsa. Kuna Tyrone Mings na Ollie Watkins pia. Ndiyo ipo hivyo."

Martinez amekuwa kwenye kikosi cha Aston Villa kwa miaka minne baada ya kujiunga na miamba hiyo akitokea Arsenal na amefanikiwa kuisaidia timu hiyo ya Villa Park kushiriki mikikimikiki ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Kwenye mechi za kwanza msimu huu, kocha Emery alimweka kando na kumpanga Marco Bizot baada ya Muargentina huyo kuwa kwenye huzuni kubwa ya kukwama kwa dili lake la kutimkia Man United.

Kocha wa Man United, Ruben Amorim baada ya kumkosa Martinez aliamua kwenda kunasa huduma ya kipa Senne Lammens kutoka Royal Antwerp.