Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha asababisha mpasuko Spurs

Muktasari:

  • Postecoglou alifutwa kazi katika mwaka wake wa pili ikiwa ni siku 16 tu baada ya kuiongoza timu hiyo kutwaa taji lake la kwanza la Ulaya baada ya miaka 41, pia taji la kwanza kwenye timu baada ya miaka 16.

LONDON, ENGLAND: TAARIFA za ndani kutoka Tottenham, zinaeleza wachezaji wa timu hiyo wamekasirishwa na kuondolewa kwa kocha wao Ange Postecoglou.

Postecoglou alifutwa kazi katika mwaka wake wa pili ikiwa ni siku 16 tu baada ya kuiongoza timu hiyo kutwaa taji lake la kwanza la Ulaya baada ya miaka 41, pia taji la kwanza kwenye timu baada ya miaka 16.

Kocha huyu alirejea kutoka likizo Ugiriki na kukutana na taarifa hiyo, huku Spurs ikieleza uamuzi huo ulifikiwa baada ya mapitio ya matokeo ya msimu uliopita na ‘tafakuri kubwa’.

Mwenyekiti Daniel Levy alifanya kikao usiku kucha baada ya mechi ya mwisho ya Ligi Kuu msiumu uliopita na walipigwa 4-1 nyumbani na Brighton, siku tano tu baada ya furaha ya kuwafunga Manchester United kwenye fainali ya Europa League huko Bilbao.

Baadaye, Levy alisafiri kwenda Bahamas alikokutana na baadhi ya wanandugu wa familia ya Lewis, ambao ni wamiliki wakuu wa timu hiyo.

Baada ya hapo, alifanya uamuzi wa kumwachisha Postecoglou kazi, lakini uamuzi huo unadaiwa kupokelewa vibaya na wachezaji.

Ripoti kutoka tovuti ya  Telegraph, inaeleza baadhi ya wachezaji wa Tottenham wanapanga kulazimisha kuondoka kwenye timu hiyo kutokana na uamuzi huo.

Chanzo kimoja kiliiambia Telegraph: “Wachezaji wamekasirika sana kuhusu kilichotokea na jinsi kilivyokuwa. Kocha ajaye atakutana na hali ngumu.”

Baadhi ya wachezaji walitumia mitandao ya kijamii usiku wa Ijumaa kutoa heshima kwa kocha wao huyo wa zamani.

Beki wa kulia Pedro Porro alichapisha picha tatu akiwa na Postecoglou kwenye Instagram pamoja na ujumbe uliosema: “Asante kwa kila kitu, kocha. Kwa kunielekeza mapema, kunisaidia kuzoea timu na kuniamini uwanjani.

“Nitashukuru daima kwa jinsi ulivyotuongoza, kututetea na kututia moyo wakati wa mafanikio na changamoto.

“Zaidi ya yote, umetupa mojawapo ya nyakati kubwa zaidi katika historia ya timu, na kwa hilo, utaheshimiwa daima. Nakutakia kila la heri, kocha.”

Mshambuliaji Richarlison aliongeza: “Kocha, asante sana kwa kunisaidia na kuniamini wakati wa kipindi kigumu sana katika maisha yangu na taaluma yangu.

“Kila mtu anayependa Spurs atakumbuka kuwa Big Ange huwa anashinda vikombe msimu wake wa pili. Tumetengeneza historia! Asante na mafanikio mema katika safari yako! Nitakuwa nakusapoti daima.”