Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wale wakubwa wanamalizaje mtoano?

Muktasari:

  • Kuelekea mechi hizo, kompyuta ya utabiri wa mechi ya Opta imefanya imezicheza ikitoa sehemu iliyobaki ya Kombe la Dunia 2026 ikionyesha nafasi ya kila timu kufika fainali na kubeba kombe. Kuanzia raundi ya 32 hadi fainali, mfumo wa Opta umetoa utabiri kamili wa Kombe la Dunia 2026, ikiwa ni pamoja na uwezekano wa kila timu kusonga mbele katika kila hatua na hatimaye kubeba kombe.

BOSTON, MAREKANI: KUNA mengi yanaendelea katika michuano ya Kombe la Dunia 2026 inayopigwa Canada, Mexico na Marekani. Achana na matokeo ya jana ya DR Congo ilivyopoteza dhidi ya Canada katika mchezo wa kwanza wa hatua ya 32 bora. Pia weka kando mechi tatu zilizopigwa usiku wa kuamkia leo kati ya Brazil na Japan, Ujerumani na Paraguay pamoja na ile ya Uholanzi na Morocco, lakini zinangatia zinazopigwa kuanzia leo usiku.

Kuelekea mechi hizo, kompyuta ya utabiri wa mechi ya Opta imefanya imezicheza ikitoa sehemu iliyobaki ya Kombe la Dunia 2026 ikionyesha nafasi ya kila timu kufika fainali na kubeba kombe. Kuanzia raundi ya 32 hadi fainali, mfumo wa Opta umetoa utabiri kamili wa Kombe la Dunia 2026, ikiwa ni pamoja na uwezekano wa kila timu kusonga mbele katika kila hatua na hatimaye kubeba kombe.

Muundo uliopanuliwa, ulioruhusu timu nane bora zilizoshika nafasi ya tatu kufuzu ulipunguza kwa kiasi fulani ushindani mkali wa hatua ya makundi, huku Uruguay ikiwa ndiyo timu pekee kubwa iliyotolewa mapema katika mazingira ya kushangaza.

Idadi kubwa ya vigogo waliotarajiwa kabla ya mashindano imefanikiwa kusonga mbele, ingawa droo ya mtoano imekuwa tofauti sana kulingana na upande wa droo timu zilipoangukia. Na sasa kwa kuwa raundi ya 32 imeshaanza, unaweza kuangalia utabiri wa mtoano wa kompyuta hiyo unaoonyesha ni timu zipi ndizo zinazopewa nafasi kubwa ya kubeba kombe Julai 19 ukizingatia zile ambazo mpaka leo hazijacheza.

Ufaransa ilianza mashindano ikiwa ya pili kwa nafasi ya kutwaa ubingwa katika utabiri wa kabla ya mashindano, ikiwa na nafasi ya asilimia 13.0. Baada ya hatua ya makundi ya kuvutia, sasa imepanda na kushika nafasi ya kwanza kwa asilimia 18.7.

Les Bleus wamekuwa timu bora zaidi katika mashindano hadi sasa, na ni moja kati ya timu tatu pekee pamoja na Argentina na Mexico  zilizoshinda mechi zote tatu za makundi. Ni mara ya kwanza kwa Ufaransa kushinda mechi zote za makundi katika mashindano makubwa tangu Kombe la Dunia 1998, ilipokwenda mbali zaidi na kubeba ubingwa ikiwa nyumbani.

Kwa mujibu wa utabiri wa hivi karibuni wa hatua ya mtoano, Ufaransa iko katika nafasi nzuri ya kuendeleza safari yake. Inatarajiwa kuishinda Sweden katika raundi ya 32, kabla ya huenda kukutana na Ujerumani katika robo fainali. Baada ya hapo, njia yao inafunguka hadi uwezekano wa nusu fainali dhidi ya Hispania.

Argentina ndiyo imefaidika zaidi na droo, huku kikosi hicho cha kocha Lionel Scaloni kikiwa sasa katika nafasi ya pili kwa nafasi ya ubingwa kwa asilimia 16.3. Safari ya kihistoria ya Cape Verde imekuwa moja ya hadithi bora za mashindano hayo, lakini kwa upande wa Argentina ni droo rahisi ya raundi ya 32. Wakisonga mbele, watakutana na Australia au Misri katika 16 bora, kisha uwezekano wa robo fainali dhidi ya Uswisi, Algeria, Colombia au Ghana. Inaonekana hadi nusu fainali ndipo Argentina watakutana na kipimo cha kweli, ambapo Brazil au England huenda wakawa wapinzani wao.

Kwa upande wa Hispania waliingia mashindanoni wakiwa vinara katika utabiri wa kabla ya mashindano wa Kombe la Dunia 2026, na ingawa wameshuka hadi nafasi ya tatu kwa asilimia 13.5, bado wako miongoni mwa timu zinazotajwa kuwa na nafasi kubwa ya kubeba ubingwa.

Mchezo wa mapema wa 16 bora dhidi ya Ureno unaonekana kuwa mgumu kuliko ilivyotarajiwa kufika mapema hivyo, lakini Hispania bado wanapewa nafasi kubwa ya kushinda. Wakisonga mbele, watakutana na moja kati ya Marekani, Bosnia-Herzegovina, Ubelgiji au Senegal katika robo fainali.

Nao England wana nafasi ya asilimia 9.7 ya kushinda mashindano katika utabiri wa hivi karibuni wa kompyuta ya Opta. Wao ni vigogo wanaopigiwa upatu kuishinda DR Congo katika raundi ya 32. Hata hivyo, njia yao inakuwa ngumu haraka. Mechi inayowezekana ya 16 bora dhidi ya Mexico huko Azteca inakaribia, ikifuatiwa na uwezekano wa robo fainali dhidi ya Brazil mjini Miami. England hawajapoteza katika mechi 11 za mashindano chini ya kocha Thomas Tuchel wakishinda 10 na sare moja, lakini watahitaji kuboresha kiwango chao baada ya hatua ya makundi iliyokuwa na mabadiliko ya hapa na pale.

Wenyeji wote watatu bado wapo kwenye mashindano na wanatarajiwa kusonga mbele kutoka raundi ya 32, kulingana na utabiri wa kompyuta ya Opta, lakini safari zao huenda zisidumu kwa muda mrefu zaidi. Marekani inapewa nafasi ya asilimia 42.5 kufika robo fainali, ikiwa ni utabiri mkubwa zaidi kati ya wenyeji hao watatu. Mexico wana asilimia 28.3, wakati Canada wanakadiriwa kuwa na asilimia 25.2 ya kufika hatua ya robo fainali.