Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kiungo ghali akosa mechi Liverpool

KIUNGO Pict

Muktasari:

  • Mjerumani huyo, anayeshikilia rekodi ya uhamisho Uingereza baada ya kunaswa kwa Pauni 116 milioni, ndiye pekee kati ya nyota sita wapya waliosajiliwa na Liverpool dirisha hili waliokosa mchezo huo wa kirafiki uliocheza uwanjani Deepdale kwa mara ya kwanza tangu kifo cha staa wao, Diogo Jota.

LIVERPOOL, ENGLAND: STAA ghali Ligi Kuu England, Florian Wirtz amekosa mechi ya kwanza ya klabu yake ya Liverpool ilipokipiga na Preston North End, ikiwa ni ya kuanza maandalizi ya pre-season.

Mjerumani huyo, anayeshikilia rekodi ya uhamisho Uingereza baada ya kunaswa kwa Pauni 116 milioni, ndiye pekee kati ya nyota sita wapya waliosajiliwa na Liverpool dirisha hili waliokosa mchezo huo wa kirafiki uliocheza uwanjani Deepdale kwa mara ya kwanza tangu kifo cha staa wao, Diogo Jota.

Kipa mwili jumba, Giorgi Mamardashvili, alinaswa kwa Pauni 29 milioni kutokea Valencia, alianzishwa golini, huku wachezaji wengine wapya Jeremie Frimpong na Milos Kerkez, pamoja na makipa Freddie Woodman na Armin Pesci, walikuwa kwenye benchi.

Lakini, kiungo Wirtz alikuwa miongoni mwa wachezaji kadhaa wa kikosi cha kwanza ambao hawakucheza mechi hiyo, ikiwamo nahodha Virgil van Dijk, Ibrahima Konate na mastaa watatu wa Amerika Kusini, Alexis Mac Allister, Luis Diaz na Alisson.

Harvey Elliott, baada ya kutamba na England Under-21 kwenye michuano ya ubingwa wa Ulaya, alipewa siku zaidi za kupumzika sambamba na Tyler Morton.

Wirtz alikuwa akifanya mazoezi ya kivyake huko Kirkby kujaribu kujiweka fiti baada ya kujiunga na timu hiyo akitokea kuitumikia Ujerumani kwenye Nations League baada ya msimu mrefu wa kuitumikia Bayer Leverkusen kwenye Bundesliga.

Liverpool ilitumia mechi hiyo pia kutuma ujumbe muhimu kwa staa wao Diogo Jota, ambaye alifariki dunia kwa ajali ya gari akiwa na mdogo wake, Andre Silva huko Hispania, Alhamisi, Julai 3. Kabla ya mechi nyimbo za ‘You’ll Never Walk Alone’ wa Liverpool na ule wa Preston ‘Can’t Help Falling In Love With You’ ziliimbwa uwanjani hapo na mwimbaji Claudio Rose Maguire, mke wa mchezaji wa zamani wa Preston, Sean.

Kulikuwa na wasiwasi wa kuhusu kufanyika kwa mchezo huo kwa sababu kulikuwa na wachezaji kadhaa wa Liverpool waliokwenda kuhudhuria maziko ya Jota, Jumamosi iliyopita, ambao walipewa muda wa ziada wa kupumzika kabla ya kurudi mazoezini.