Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kisa umaarufu, McTominay ataka kurudi England

MC Pict

Muktasari:

  • Kiungo huyo wa zamani wa Manchester United, aliiongoza Napoli kutwaa ubingwa wa Serie A msimu uliopita, akihusika kwa asilimia kubwa kutokana na kiwango chake.

NAPLES, ITALIA: KIUNGO wa Napoli na timu ya taifa ya Scottland, Scott McTominay inadaiwa anaweza kurejea Ligi Kuu England mwakani kutokana na changamoto nyingi anazopitia nje ya Uwanja zinazosababishwa na umaarufu wake katika Jiji la Naples yalipo makao makuu ya Napoli.

Kiungo huyo wa zamani wa Manchester United, aliiongoza Napoli kutwaa ubingwa wa Serie A msimu uliopita, akihusika kwa asilimia kubwa kutokana na kiwango chake.

McTominay, 28, alifunga mabao 12 katika msimu wake wa kwanza na kuchaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Mwaka wa klabu hiyo, huku pia akimaliza nafasi ya 18 kwenye tuzo za Ballon d’Or.

Msimu huu amefunga mabao matatu na Napoli imekuwa ikipambana kupata matokeo kwa sasa ikiwa nafasi ya tatu, pointi mbili nyuma ya vinara AC Milan.

MCT 01

Chanzo kimoja kiliiambia tovuti ya The Sun:"Scott anapenda baadhi ya vitu katika maisha yake hapa Italia. Mashabiki wanampenda sana kutokana na kiwango alichoonyesha msimu uliopita lakini upendo huo kuna wakati huwa ni kero kwake. Anatazamwa sana hali inayosababisha iwe ngumbu kwake kufanya vitu rahisi nje ya Uwanja."

Inaelezwa Scott huwa anapata changamoto hata anapohitaji kutembea tu, huwa ni shida kwani popote mashabiki wanapomwona huwa wanamsimamisha, baadhi wakitaka kupiga naye picha na wengine wakitaka awasainie jezi zao.

MCT 02

Inaelezwa hiyo ni tofauti na alipokuwa England ambako licha ya kuwa mmoja ya wachezaji wa timu kubwa, mashabiki hawakuwa wanamtazama sana.

Napoli, ambayo ilimsajili Kevin De Bruyne kutoka Manchester City dirisha lililopita la majira ya kiangazi ili kuongeza nguvu katika eneo la kiungo, wiki iliyopita iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Inter Milan katika mechi iliyokuwa na ushindani wa aina yake ikiwa ni baada ya kupokea kichapo kizito cha mabao 6-2 kutoka kwa PSV katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.