Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kinda Lewis-Skelly mwanzo mzuri

Muktasari:

  • Beki huyo wa pembani wa Arsenal alifunga bao hilo dhidi ya Albania ikiwa ni mechi yake ya kwanza kuchezea kikosi cha wakubwa cha Three Lions.

LONDON, ENGLAND: KINDA wa Arsenal, Myles Lewis-Skelly ameweka rekodi ya kucheza mechi yake ya kwanza kwenye timu ya taifa ya England na kisha kufunga bao katika mechi hiyo ya kimashindano.

Beki huyo wa pembani wa Arsenal alifunga bao hilo dhidi ya Albania ikiwa ni mechi yake ya kwanza kuchezea kikosi cha wakubwa cha Three Lions.

Akiwa na umri wa miaka 18 na siku 176, amekuwa mchezaji mwenye umri mdogo kufunga bao kwenye mechi yake ya kwanza ya kuitumikia England.

Lewis-Skelly amevunja rekodi iliyokuwa imewekwa na Marcus Rashford - ambaye aliweka akiwa na umri wa miaka 18 na siku 209 katika mechi dhidi ya Australia, Mei 2016.

Bao la Lewis-Skelly lilikuwa la kwanza kwa England ikiwa chini ya kocha Mjerumani, Thomas Tuchel tangu aliporithi mikoba kutoka kwa Sir Gareth Southgate.

Tuchel alimzungumzia Lewis-Skelly akisema: “Tumevutiwa na Myles tangu alipoanza kucheza, amekuwa panga pangua kwenye kikosi cha Arsenal, ni mchezaji mzuri na Mikel Arteta amekuwa akimchagua na kumwaanzisha.”

Bao la Lewis-Skelly ilikuwa ni asisti ya Jude Bellingham kabla ya straika Harry Kane kufunga la pili kwenye mechi hiyo ya ushindi wa mabao 2-0 baada ya pasi maridadi ya kiungo Declan Rice.