Kinanuka leo UEFA

DORTMUND, UJERUMANI. BAADA ya kusubiriwa kwa hamu sasa michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya imerejea tena na leo Machi 9, 2021 kutakua na michezo miwili ya mkondo wa pili hatua ya 16 bora ambapo Borussia Dortmund ikiwa nyumbani itailakika Sevilla wakati Juventus ikiialika FC Porto mechi zote zitapigwa saa 5:00 usiku.
Dortmund inaingia kwenye mechi hiyo ikiwa na matumaini makubwa ya kusonga mbele kwa sababu ilishinda mchezo wa kwanza kule Hispania kwa mabao 3-2.
Hivyo, kwenye mechi hiyo inahitaji kutoa sare ama kushinda bao moja na kusonga kwenye hatua ya robo fainali.
kimbembe kitakua kwa Sevilla ambayo itatakiwa kushinda mabao yasiyopungua mawili ili kusonga mbele.
Mchezo mwingine kwa leo utakua kati ya Juventus na Porto na hapa Juve ndio inahitaji zaidi kushinda kwa sababu mchezo wa kwanza uliopigwa kule Ureno ilikubali kichapo cha mabao 2-1.
Ikiwa itafanikiwa kushinda 1-0 itakua imefanikiwa kupita lakini sare yoyote ya mabao itakua inawaondoa kwenye michuano hiyo.
Porto imekua haina kiwango kizuri kwenye siku za hivi karibuni ambapo michezo yake mitatu ya mwisho imeshinda moja, sare moja na kufungwa moja.