Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kimeo cha jezi Namba 7 kinavyotisha Man United

Muktasari:

  • Tangu Cristiano Ronaldo alipouzwa kwa pesa nyingi kwenda Real Madrid mwaka 2009, mchezaji aliyefanya vizuri akiwa na jezi hiyo Namba 7 ni Cristiano Ronaldo mwenyewe.

MANCHESTER, ENGLAND: STAA wa Manchester United, Mason Mount anapambana kwa nguvu kujiondoa kwenye gundu linalowaandama mastaa wengi waliokabidhiwa jezi Namba 7 kwenye kikosi.

Tangu Cristiano Ronaldo alipouzwa kwa pesa nyingi kwenda Real Madrid mwaka 2009, mchezaji aliyefanya vizuri akiwa na jezi hiyo Namba 7 ni Cristiano Ronaldo mwenyewe.

Ronaldo aliporudi Man United kwa mara ya pili mwaka 2021 alipata mafanikio kama mchezaji binafsi, ambapo alifunga mabao 24 katika msimu ambao alitimiza umri wa miaka 37, lakini kiwango kibaya kwa timu nzima kiliifanya miamba hiyo ya Old Trafford kumaliza nafasi ya sita.

Katikati ya awamu hizo mbili za Ronaldo kwenye kikosi cha Man United, wachezaji wengine waliowahi kuvaa jezi Namba 7 ni Michael Owen, Antonio Valencia, Angel di Maria, Memphis Depay, Alexis Sanchez na Edinson Cavani. Wote hao, hakuna aliyetoboa akiwa na Namba 7 mgongoni kwenye jezi yake.

Owen alichemsha, Valencia aliomba kubadilisha na kurudi kwenye Namba 25 aliyokuwa akivaa awali baada ya Namba 7 kuwa nzito kwake, Angel di Maria aliondoka Man United baada ya mwaka mmoja tu kutokana na kuonyesha kiwango cha hovyo, huku Depay alikomea miezi 18 tu kwenye timu hiyo na Sanchez hakuwa na maajabu yoyote.

Cavani alifunga mabao 17 akiwa na jezi Namba 7, lakini alisumbuliwa sana na majeraha ya mara kwa mara na kumfanya akose mechi kibao.

Hadi kufikia msimu huu, Mason Mount naye alikuwa kwenye wakati mgumu wa kujinasua kwenye gundu linalotokana na kuvaa jezi Namba 7, ambayo ilivaliwa na magwiji wa Man United kama George Best, Bryan Robson, Eric Cantona na David Beckham.

Mount, aliposajiliwa mwaka 2023 kwenda kucheza kiungo ya kati, kwenda kuwa mchezeshaji wa kikosi hicho, nafasi ambayo alicheza kwenye mechi mbili tu.

Baada ya hapo, Mount amekuwa akibadilishwa tu mara kushoto, wakati mwingine kulia na alikuwa akicheza pia kati Man United ilipokuwa chini ya kocha Erik ten Hag. Lakini, Mount alikosa mechi 31 msimu wa kwanza na mechi 30 uliopita, akiwa na uzi huo wa Man United wenye Namba 7 mgongoni.