Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Keane, Neville, Carragher waonywa kuhusu City

Muktasari:

  • Hukumu ya suala hilo baina ya Ligi Kuu England na Man City inatarajiwa kutolewa wiki chache zijazo.

LONDON, ENGLAND: SKY Sports imeonya wachambuzi wake jinsi inavyochambua kwa mbwembwe bila ya kufuata weledi juu ya sakata la mashtaka 115 yanayoikabili Manchester City juu ya madai ya udanganyifu kwenye matumizi.

Hukumu ya suala hilo baina ya Ligi Kuu England na Man City inatarajiwa kutolewa wiki chache zijazo.

Mabosi wa Sky wanataka jambo hilo liripotiwe kwa kufuata weledi kwa maana ya kubainisha vitu kwa usahihi, usawa na haki. Na kutokana na hilo, imewaambia wachambuzi wake wasijadili kishabiki.

Kwenye hilo, mabosi wa Sky wanaripotiwa kuwachapa barua wachambuzi wao maarufu akiwamo Gary Neville, Jamie Carragher na Roy Keane, ikiwataka kuwa na takwimu za kutosha juu ya jambo hilo na waeleze kinachotakiwa kuelezwa bila ya kuongeza kitu chochote kwa hisia zao.

Man City imekumbana na mashtaka 115 ya kudaiwa kukiuka kanuni za usawa kwenye mapato na matumizi.

Mabingwa hao wa Ligi Kuu England, ambao wamekana kutenda kosa lolote kwenye mashtaka hayo, wameongezewa mashtaka mengine 15 na kufanya jumla kuwafanya kukabiliwa na mashtaka 130.

Man City ilitumia Pauni 175 milioni kwenye usajili wa nyota wapya katika dirisha la Januari.

Endapo kama Man City itakutwa na hatia kwenye mashtaka hayo, basi adhabu inayowakabili inaweza kuwa kupokwa pointi, kupigwa faini na hata kushushwa daraja.