Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bosi Arsenal apanda ndege kumfuata Gyokeres

Arsenal Pict

Muktasari:

  • Baada ya wiki kadhaa za uvumi mwingi  kuhusu mastraika Gyokeres na Benjamin Sesko, ikafahamika wazi kwamba Arsenal nguvu yao ipo kwenye usajili wa staa wa kimataifa wa Sweden, ambaye ameonyesha dhamira ya wazi kutaka kuondoka Sporting baada ya msimu mzuri Primeira Liga.

LONDON, ENGLAND: BOSI wa usajili kwenye kikosi cha Arsenal, Andrea Berta amekwea pipa kwenda Ureno kufanya mazungumzo ya kina na mabosi wa Sporting Lisbon kwa ajili ya kukamilisha usajili wa straika wa mabao, Viktor Gyokeres.

Baada ya wiki kadhaa za uvumi mwingi  kuhusu mastraika Gyokeres na Benjamin Sesko, ikafahamika wazi kwamba Arsenal nguvu yao ipo kwenye usajili wa staa wa kimataifa wa Sweden, ambaye ameonyesha dhamira ya wazi kutaka kuondoka Sporting baada ya msimu mzuri Primeira Liga.

Mazungumzo ya kumleta Gyokeres kwenye kikosi cha Arsenal ni mchakamchaka wa timu hiyo kwenye msako wao wa Namba 9 mpya unaelekea kukamilika. Na sasa imethibitika kwamba Berta, mkurugenzi wa michezo mpya wa Arsenal amesafiri kwenda Ureno kukutana ana kwa ana na mabosi wa Sporting ili kukamilisha dili la kumnasa straika huyo kwa dili linaloaminika litagharimu Pauni 70 milioni. Berta alienda Ureno mwishoni mwa wili iliyopita, inaaminika alirudi England na sasa amerudi tena Ureno kukamilisha dili hilo. Safari yake hiyo inamaanisha kwamba Arsenal itaka kukamilisha dili la kumsajili straika huyo, ambaye hajawahi kuwa na shida ya kufunga, akitikisa nyavu mara 54 kwenye kikosi cha Sporting msimu uliopita.

Kinaelezwa ni kwamba Arsenal imeshafikia makubaliano ya maslahi binafsi ya mchezaji huyo, ambapo Gyokeres atasaini mkataba wa miaka mitano utakaomshuhudia akilipwa Pauni 200,000 kwa wiki.

Kocha Mikel Arteta anahitaji straika mpya atue kwenye kikosi chake kabla ya kuanza kwa ziara za pre-season, akipanga kufanya vizuri kwenye Ligi Kuu England msimu ujao baada ya kumaliza nafasi ya pili kwa misimu mitatu mfululizo.

Miamba hiyo ya Emirates tayari imeshawanasa kipa Kepa Arrizabalaga na kiungo Martin Zubimendi huku ikiwa kwenye hatua nzuri ya kukamilisha dili la kiungo mwingine, Christian Norgaard. Ikikakamilisha usajili wa Gyokeres, itahamia kwa winga, ikiwasaka Rodrygo, Noni Madueke na Eberechi Eze.