Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kazini kwa Gyokeres kuna kazi

Muktasari:

  • Gyokeres alikuwa chaguo la kocha Mikel Arteta katika dirisha lililopita la majira ya kiangazi wakati alipokuwa akitafuta mshambuliaji wa maana kufuatia miaka kadhaa ya kucheza bila ya kuwa na Namba 9 wa uhakika. Hili lilionekana kama udhaifu mkubwa wa Arsenal na ilitumia zaidi ya Pauni 60 milioni kumsajili Gyokeres kutoka Sporting Lisbon ya Ureno.

LONDON, ENGLAND: STRAIKA Viktor Gyokeres ni rahisi tu kusema kazini kwake kuna kazi baada ya magwiji tofauti wa Ligi Kuu England kumsakama wakidai “hana kile kinachohitajika” kuifanya Arsenal iwe mabingwa, kwa mujibu wa Dietmar Hamann, ambaye anadai kuwa mshambuliaji huyo “si mzuri vya kutosha” kuiongoza safu ya ushambuliaji ya klabu hiyo.

Gyokeres alikuwa chaguo la kocha Mikel Arteta katika dirisha lililopita la majira ya kiangazi wakati alipokuwa akitafuta mshambuliaji wa maana kufuatia miaka kadhaa ya kucheza bila ya kuwa na Namba 9 wa uhakika. Hili lilionekana kama udhaifu mkubwa wa Arsenal na ilitumia zaidi ya Pauni 60 milioni kumsajili Gyokeres kutoka Sporting Lisbon ya Ureno.

Mshambuliaji huyo alikuwa amefunga mabao 97 katika misimu miwili aliyokaa Ureno, lakini ameshindwa kuonyesha kiwango hicho katika Ligi Kuu England, licha ya Arsenal kuwa kileleni mwa msimamo wa ligi. Amekosolewa sana kwa kushindwa kuzoea ligi mpya, huku mabao yakiwa machache.

Gyokeres amefunga mabao 10 katika mechi 29 alizoichezea Arsenal, ambapo mabao matano tu yametoka kwenye Ligi Kuu. Aidha, hana bao lolote la kawaida (lisilo la penalti) katika mechi 11 zilizopita za ligi.

Na sasa, nyota wa zamani wa Liverpool, Hamann, amefikia hitimisho kwamba Gyokeres hayuko katika kiwango cha Arsenal.

Akizungumza na CasinoBeats, alisema: “Nilisema mara nyingi kuwa Arsenal walihitaji mshambuliaji wa kati. Kwa sasa, hata kama Viktor Gyokeres hakuanza mwishoni mwa wiki, sidhani kama ni mmoja wa washambuliaji bora barani Ulaya. Anaweza kufunga mabao, lakini dhidi ya timu bora, hilo pekee halitoshi kwa sababu sidhani kama atajikuta katika nafasi nyingi za kufunga.

“Walimsajili Gyokeres kama mshambuliaji wa kati, lakini sidhani kama ni mzuri vya kutosha. Kama hilo litakuwa sababu ya kuamua hatima yao mwishoni mwa msimu sijui, lakini kwa sasa halijasaidia Arsenal.”


Tumemwona Gyokeres katika klabu kadhaa kabla ya Sporting, na sina uhakika kama ana uwezo wa kucheza dhidi ya mabeki bora barani Ulaya na katika Ligi Kuu.”

Mjerumani huyo amesisitiza kuwa wachezaji wapya wanahitaji kupewa muda, lakini bado haamini Gyokeres anaweza kuipeleka Arsenal inakotaka kuwa.

Aliongeza: “Wakati mwingine tunapaswa kuwapa wachezaji muda kwa sababu mpira ni mchezo mgumu. Lakini, kwa uaminifu, sina uhakika kama ana kile kinachohitajika kuiongoza safu ya ushambuliaji ya klabu kama Arsenal na kuwasaidia kutwaa ubingwa.”

Arsenal ilikuwa na mechi ya ugenini dhidi ya Leeds United kwenye Ligi Kuu England, ambapo Gyokeres alitarajia kufanya makubwa kusaidia timu.