Kane afunguka kuondoka Bayern Munich

Muktasari:
- Katika uhamisho wake wa Pauni 120 milioni, kapteni huyo wa England aliwekewa kipengele ambacho kinamruhusu Januari ya mwaka huu ambapo ilitakiwa timu inayomhitaji kulipa Pauni 67 milioni ili kumpata kiasi ambacho kitapungua kufikia Pauni 54 milioni Januari mwakani.
MUNICH, UJERUMANI: STRAIKA wa Bayern Munich, Harry Kane amefunguka kuhusu mustakabali wake kwenye kikosi cha Bayern Munich baada ya kugundulika kuwa na kifungu katika mkataba wake ambacho kitamwezesha kuondoka Januari mwakani.
Katika uhamisho wake wa Pauni 120 milioni, kapteni huyo wa England aliwekewa kipengele ambacho kinamruhusu Januari ya mwaka huu ambapo ilitakiwa timu inayomhitaji kulipa Pauni 67 milioni ili kumpata kiasi ambacho kitapungua kufikia Pauni 54 milioni Januari mwakani.
Kane alifunga mabao mawili kwenye ushindi wa 3-0 wa Bayern dhidi ya Werder Bremen nyumbani Ijumaa na kiujumla amefunga mabao 21 katika mechi 19 za ligi msimu huu.
Wiki iliyopita pia aliweka rekodi ya kufunga mabao 20 au zaidi katika msimu mmoja kwa mara ya nane katika maisha yake ya soka, akimzidi Alan Shearer ambaye alifanya hivyo kwa misimu saba.
Hata hivyo, akizungumza baada ya mchezo, Kane alijizuia kutoa maelezo kuhusu mkataba wake na alikataa kuzungumzia hatma yake pia.
"Sitaki kuzungumzia hilo. Ninachoweza kusema ni kwamba ni furaha kubwa kuwa ndani ya FC Bayern," alisema Kane alipohojiwa na Sky Sports Germany.
Kifungu hicho kinaweza kutumika pale tu Bayern itakapokubali kumuuza Kane na mshambuliaji huyo akatoa idhini ya kuondoka.
Hata hivyo, katika mkataba huo, timu ya kwanza ambayo Bayern inatakiwa iipe nafasi ya kumnunua ikiwa inahitaji kumuuza Kane ni Spurs ingawa hakuna kiasi maalumu kilichowekwa.
Vilevile kama timu yoyote itafikia makubaliano ya kutumia kipengele kilichopo katika mkataba huo ili kumpata Kane Spurs itakuwa na haki ya kuingilia kati na kulipa kiasi sawa na hicho na kumsajili fundi huyo wa kimataifa wa England.
Hadi anaachana na Bayern, Kane alikuwa amefunga mabao 213 ya Ligi Kuu England ikiwa ni pungufu ya mabao 47 nyuma ya mfungaji bora wa muda wote Alan Shearer.
Licha ya uwezekano wa kuondoka, watu wa karibu na mshambuliaji huyu wamefunguka kwamba hana mpango wa kufanya hivyo na anafurahia maisha katika Jiji la Munich