Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha wa viungo Morocco afichua maumivu aliyopitia Brahim Diaz

DIAZ Pict

Muktasari:

  • Diaz alijaribu kupiga penalti ya mtindo wa ‘Panenka’ lakini jaribio hilo halikufanikiwa na kumuacha akiwa hana furaha kwa siku kadhaa. 

Kocha wa viungo wa timu ya taifa ya Morocco, Eduardo Dominguez, amefunguka kuhusu athari za kihisia alizopitia nyota wa timu hiyo, Brahim Diaz, baada ya kukosa penalti katika mechi ya fainali ya AFCON 2025 dhidi ya Senegal.

Diaz alijaribu kupiga penalti ya mtindo wa ‘Panenka’ lakini jaribio hilo halikufanikiwa na kumuacha akiwa hana furaha kwa siku kadhaa. 

Akizungumza na kipindi cha redio cha El Larguero, Dominguez ameeleza tukio hilo lilikuwa na maumivu makali. Kwa mujibu wa Dominguez, baada ya mechi kumalizika, kikosi kilirejea kimya kimya huku kikiwa katika hali ya mshangao na sintofahamu. 

“Hakuna aliyekuwa akijua nini kingefuata,” amesema. 

Kumbukumbu yake ya mwisho juu ya Diaz ilikuwa uwanja wa ndege, ambapo mchezaji huyo alionekana kubeba mzigo mzito wa kihisia. 

“Hakuna maneno mengi ya kumwambia mtu anayebeba uzito huo akilini,” amekiri.

Penalti hiyo aliyokosa imekuwa moja ya matukio makubwa yaliyotawala mashindano hayo. Diaz alikuwa mchezaji tegemeo wa Morocco, akifunga mabao matano na kuiongoza timu hiyo kufika fainali kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2004. Nafasi ya kuipa nchi ubingwa wa kwanza tangu 1976 ilitoweka baada ya jaribio hilo la Panenka kwenda kombo.

Hata hivyo, licha ya tukio hilo, hadhi ya Diaz haikuyumba. Uchezaji wake wa kiwango cha juu ulimfanya kuwa miongoni mwa wachezaji bora wa mashindano, huku rekodi ya kutopoteza mechi 32 mfululizo chini ya kocha Walid Regragui ikiongeza uzito wa matarajio katika fainali hiyo.

Fainali ya 2025 pia itakumbukwa kwa matukio ya nje ya uwanja. Timu ya Senegal ilitoka uwanjani kupinga uamuzi wa penalti uliothibitishwa na VAR, jambo lililosababisha vurugu na uharibifu wa mali. Mahakama ya Morocco tayari imewahukumu mashabiki 18 waliokamatwa vifungo vya kati ya miezi mitatu hadi mwaka mmoja jela.

Wakati huo huo, Shirikisho la Soka Afrika (CAF), limemfungia kocha wa Senegal, Pape Bouna Thiaw, mechi tano pamoja na kumtoza faini ya dola 100,000 (Sh260 milioni).

Kwa maana hiyo, fainali ya AFCON 2025 imeacha kumbukumbu yenye mchanganyiko wa majonzi na mafanikio, maumivu binafsi ya Diaz, ndoto za taifa zilizoyeyuka, na athari zinazoendelea kufuatia matukio yaliyoizunguka mechi hiyo.