Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kai Rooney aanzia alipoishia baba'ke

Muktasari:

  • Kampuni hiyo ambayo inamsimamia Kai (16) ambaye ni mtoto wa gwiji wa klabu hiyo, Wayne Rooney ndani na nje ya uwanja, inataka kumfanya kinda huyo kuwa na mafanikio ya kiuchumi.

MANCHESTER, ENGLAND: KINDA wa Manchester United, Kai Rooney anatarajiwa kuanza kupokea hadi Pauni 3 milioni baada ya kusaini mkataba mpya na kampuni ya Triple S Sports Management wiki hii utakaomwongezea thamani katika klabu hiyo.

Kampuni hiyo ambayo inamsimamia Kai (16) ambaye ni mtoto wa gwiji wa klabu hiyo, Wayne Rooney ndani na nje ya uwanja, inataka kumfanya kinda huyo kuwa na mafanikio ya kiuchumi.

Akizungumzia hilo, Profesa Jonathan Shalit, mwenyekiti wa shirika la vipaji la InterTalent, anaamini Kai atafikia hadhi ya kuwa milionea baada ya kusaini mkataba na kampuni hiyo.

Mshambuliaji huyo kwa sasa anasimamiwa na kampuni hiyo ambayo iliwahi kufanya kazi na Rooney na inamilikiwa na wakala wa muda mrefu wa baba yake, Paul Stretford.

Habari za Kai kujiunga na kampuni hiyo zilitangazwa kupitia Instagram kwa ujumbe uliosema: “Tuna furaha kutangaza kusaini kwa @kairooney.10 kujiunga na Triple S Sports! Tunafurahia kuanza kufanya kazi na mshambuliaji wa Manchester United huku akiendelea na safari yake katika soka. Mustakabali mzuri uko mbele. Karibu kwenye timu, Kai!”

Akiwa tayari anang’ara katika kikosi cha vijana chini ya miaka 18 cha United, Kai amewavutia wengi Old Trafford na kulingana na Profesa Shalit, ambaye aliwahi kuwawakilisha mastaa wa muziki kama Sting na Cher, uamuzi huu wa hivi karibuni utamletea mapato makubwa.

Shalit aliiambia Manchester Evening News: “Tayari (Kai) anatimiza vigezo vingi, hivyo nadhani ndani ya mwaka mmoja ujao anaweza kupata Pauni 2 milioni hadi 3. Nafikiri kwa sababu anaitwa Rooney atapata wafuasi milioni mara moja.

"Na bila shaka anacheza katika moja ya klabu bora duniani. Kutoka kwenye historia ya wazazi wake na kuchezea klabu kubwa kunampa thamani ya haraka ambayo kawaida kijana asingekuwa nayo.”

Profesa Shalit alisisitiza Kai anaweza kwa urahisi kupata mikataba ya matangazo na njia ya Wayne katika uchambuzi wa soka pamoja na umaarufu wa mama yake Coleen katika televisheni vinaweza kuimarisha taswira ya kibiashara.

“Kai anaweza haraka sana kutangaza bidhaa za michezo na maisha ya kawaida kwa sababu ni kijana mwenye nguvu, mchangamfu na jina la Rooney bado lina thamani kubwa,” alisema.

“Baba yake anajijenga upya kwa ustadi kama mchambuzi wa TV, mama yake anapendwa sana na ana kipaji. Asingekuwa anacheza Manchester United kwa sababu ya jina lake tu, anacheza kwa sababu ya kipaji chake.”

Ingawa nafasi anayopendelea ni winga wa kulia, Kai ameonyesha kufuata nyayo za baba yake linapokuja suala la kufunga mabao na alifunga mabao manne katika ushindi wa 6-2 wa nusu fainali ya PL Cup dhidi ya Norwich akiwa na kikosi cha chini ya miaka 16 kabla ya kupandishwa hadi U18.

Amecheza mechi tano katika kikosi hicho na zote akitokea benchi, na amefunga bao moja katika dakika 91. Pia Alipata dakika 28 za kucheza katika ushindi wa United wa 5-2 dhidi ya Nottingham Forest wiki iliyopita.