Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Juventus yampiga marufuku Dani Alves kuanzisha mazungumzo ya kusajiliwa na Chelsea, Man City

Muktasari:

Kwa mujibu wa Sky Italia, mwandishi Fabrizio Romano aliandika kwamba hata wakala wa mchezaji huyo aliyetaka kuonana na Juventus alielezwa jambo kama hilo aliloambiwa Alves.

Hispania. Klabu ya Juventus imemchimba mkwara mchezaji wake Dani Alves kwamba atalazimikiwa kujiuzulu iwapo ataanzisha mazungumzo ya kusajiliwa na klabu za Chelsea na Manchester City.

Kwa mujibu wa Sky Italia, mwandishi Fabrizio Romano aliandika kwamba hata wakala wa mchezaji huyo aliyetaka kuonana na Juventus alielezwa jambo kama hilo aliloambiwa Alves.

Alves alijiuga Seria A msimu uliopita kwa mkataba wa miaka miwili na tayari ameanza kuhusishwa kuondoka klabuni hapo. Pia anatajwa kwenda kujiunga na klabu mojawapo ya England kati ya Chelsea na Manchester City.